Kiasi kikubwa cha hasara katika ukuzaji wa mbegu hupatikana baada ya mavuno. Mbinu duni za ukaushaji na uhifadhi wa mbegu hupunguza ubora na kiasi cha mbegu za kunde.
Kunde hutumiwa na watu, hutoa kipato, na protini kwa wanyama. Kunde, karanga na soya zinaweza kutumika kama mazao ya mtego ili kudhibiti magugu ya vimelea kama vile kiduha, na kuongeza nitrojeni kwenye udongo.
Kukausha mbegu
Ukaushaji duni wa mbegu huathiri uwezo wa mbegu kuota. Kausha mbegu za kunde zilizopurwa vizuri kwa masaa 4 kwa siku 3 chini ya jua. Hifadhi mbegu kwenye chombo, juu ya ardhi.
Dumuzi wa mbegu za kunde hutaga mayai ambayo hujiingiza kwenye maganda, kisha huanguliwa na kutoboa kwenye mbegu.
Uhifadhi wa mbegu
Kwa vile dumuzi ndio wadudu wanaoathiri zaidi mbegu za kunde, kuna haja ya kupunguza uharibifu wa mbegu kwa kuepuka kuingiza wadudu hawa kwenye chumba cha kuhifadhia.
Wakati wa kuhifadhi, epuka uingizaji wa hewa na kufungua chombo ili kuzuia mayai kuanguliwa. Changanya mbegu na kichanga na majivu ili kuondoa hewa kwenye mbegu kabla ya kuhifadhi. Hii huua dumuzi, ha huzuia kujamiiana. Hatimaye, kausha mimea yenye harufu kali ili kuua au kufukuza dumuzi wakati wa kuhifadhi.