Vidukari ni wadudu wadogo, rangi ya kijani au nyeusi. Vidukari huharibu mimea kwa kunyonya maji yake, kwa hivyo hukua polepole. Vidukari pia huhamisha magonjwa ya virusi.
Jinsi vidukari wanaishi
Vidukari huishi kwa makundi. Katika jua kali, vidukari huhamia chini ya majani ili kupata kibaridi. Vidukari wakikomaa,wengine hupata mabawa na huruka kwa mimea na mashamba mengine. Vidukari hutoa kinyesi kitamu. Kinyesi hiki huitwa utomvu. Mchwa hula utonvu, na pia hupatikana kwenye majani. Jivu husaidia kufanya majani kuwa magumu. Hivyo, vidukari hawawezi tena kunyonya maji kutoka kwa majani. Vidukari hushambulia sana maharage na mboga. Mazao mengine yanaoshambuliwa ni haradali, kabichi na jani la mtambu.
Kudhibiti vidukari
Tembelea shamba lako kila mara ili kutambua vidukari. Wangamize vidukari kwa vidole. Nyunyiza majivu poa asubuhi, ili umande ufanye majivu haya yashikamane na majani. Nyunyiza majivu ya mabua ya mpunga au kuni. Kamwe, usitumie majivu ya majani ya ndizi, maharadali, mianzi na majani ya miti, kwasaba majivu haya yana nguvu sana, na yatachoma mimea ya mboga.
Unaweza pia kutumia maji ya sabuni. Sugua sabuni kwenye tungi la maji hadi litakapotoa povu. Nyunyiza maji haya shambani mara moja kila siku, kwa siku 3. Tumia mchanganyiko wa mwarobaini ili kudhibiti vidukari. Saga kilo 2 za majani ya mwarobaini na uchanganye na lita 16 za maji. Nyunyiza mchanaganyiko huo mara moja kila siku kwa siku 3.
Panda ufuta na mimea ya maharadali karibu na shamba lako. Kwa hivyo, dudu kobe huvutiwa na kula vidukari.