»Kudhibiti ugonjwa wa bakajani chelewa katika nyanya«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/managing-tomato-late-blight

Muda: 

00:08:51
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

Practical Action Nepal

Nyanya ni moja wapo ya mboga muhimu ambayo hulimwa ulimwenguni kote. Nyanya huliwa mbichi, au kupikwa kama chanzo kikuu cha vitamini, na madini.

Nyanya pia ni chanzo kizuri cha mapato kwa wakulima wengi.

Nyanya huathiriwa na wadudu wengi, na magonjwa. Bakajani chelewa ni ugonjwa haribifu.

Dalili za ugonjwa

Vidonda vyeusi vya majani ambavyo baadae hugeuka hudhurungi. Vidonda vya rangi ya hudhurungi vilivyo na majimaji hutokea juu ya matunda, na mwishowe mmea hufa.

Ugonjwa huo husababishwa na ukungu, na huenea kwa chembe za kuvu. Chembe za kuvu huhamishwa na upepo, maji ya mvua na maji machafu.

Usimamizi wa ugonjwa

Usipande mazao kama vile viazi, pilipili, biringani pamoja na nyanya kwa sababu wote huathiriwa na bakajani chelewa.

Ongeza mbolea au mboji, na chokaa ili kupunguza asidi.

Udhibiti wa ugonjwa

Panda aina sugu kama inavyoshauriwa na bwanashamba au mshauri.

Simamisha mimea ili isiguse ardhi.

Fanya ukaguzi wa kila siku shambani ili kugundua ukuepo wa ugonjwa.

Choma sehemu za mmea zilizoathiriwa. Usiweke sehemu za mmea mgonjwa kwenye mbolea.

Safisha zana au vifaa vilivyotumiwa, kwa sabuni au maji yaliyochemka ili kuua viini.

Pogoa mimea kwa kukata matawi ya chini.

Panda mimea tofuati kwa misimu tofauti ili kuangamiza mzunguko wa magonjwa.

Nyunyizia dawa ya kiasili na viuakuvu.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:48Bakajani chelewa au ugonjwa wa kuchoma ni moja wapo ya magonjwa kubwa zaidi ya nyanya.
00:4901:30Utambuzi wa magonjwa: Vidonda vyeusi kwenye majani ambayo baadaye hubadilika hudhurungi.
01:3102:07Ugonjwa huu huenea kwa mvua, upepo na maji machafu.
02:0803:17Usipande nyanya katika shamba lile lile ulilokuza mazao kama vile viazi, pilipili, biringani awlali.
03:1803:58Ongeza mbolea au mboji, na chokaa ili kupunguza asidi.
03:5904:32Panda aina sugu
04:3305:03Simamisha mimea ili isiguse ardhi
05:0405:25Kagua shamba lako, ukichoma mimea iliyoathiriwa. safisha zana, pogoa mimea, kata matawi ya chini, palilia, mwagilia maji, na nyunyiza viuakuvu vya kiasili
05:2605:42Safisha zana zako
05:4306:46Pogoa mimea, kata matawi ya chini, palilia, mwagilia maji asubuhi,
06:4707:20Nyunyiza viuakuvu vya kiasili.
07:2108:51Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *