Vitunguu hukua vizuri katika mazingira tofauti. Vitunguu hupata magonjwa zaidi wakati wa joto na unyevu. Magonjwa husambazwa na udongo, mbegu au mabaki yaliyoathiriwa.
Dalili za magonjwa ya vitunguu ni madoa ya hudhurungi, mistari ya manjano na majani kujikunja. Ili kukuza vitunguu vyenye afya, panda aina bora za mbegu kwa kutafuta ushauri kutoka kwa washauri. Nunua mbegu zilizotibiwa kutoka kwa wauzaji wanaoaminika ili kuepuka miche yenye ubora duni.
Kuzuia magonjwa
Ongeza mbolea oza kwenye kitalu ili kudumisha vitunguu vyenye afya na sugu dhidi ya magonjwa. Panda mbegu kwa mstari na acha nafasi ya kutosha ili kuwezesha upitaji mzuri wa hewa. Ondoa miche yenye magonjwa na dhaifu wakati wa kupandikiza ili kuzuia kuenea kwa magonjwa. Inua vitalu hasa wakati wa masika ili kuwezesha kutoa maji ya ziada kwa urahisi. Mwagilia maji ya kutosha, lakini epuka kumwagilia maji mengi sana. Daima, nyuyizia maji mimea asubuhi ili iwe na muda wa kukauka wakati wa mchana. Palilia mara kwa mara ili kusababisha mzunguko mzuri wa hewa.
Kukagua shamba kila wakati ni muhimu ili kutambua kwa urahisi mimea iliyoathiriwa na magonjwa. Ng‘oa vitunguu vilivyo na ugonjwa na uvizike ili kudhibiti kuenea.
Tumia mbolea za majani ili kukuza mimea thabiti, yenye afya. Tumia dawa za kuua kuvu ili kuzuia magonjwa.
Fanya mzunguko wa mazao ili kuangamiza ugonjwa. Usipande vitunguu kwenye shamba lenye ugonjwa kwa miaka 3. Ondoa mabaki ya mimea baada ya kuvuna ili kuzuia kuambukizwa tena.