Mchele wa Kiafrika ni ladha, lakini mara nyingi huuzwa kwa bei ya chini kwa sababu ya ubora duni. Ni muhimu kuboresha ubora wa mchele ili kupata pesa zaidi.
Afrika hununua kiwango kikubwa cha mchele kutoka nje, ambao mara nyingi huwa mchele uliovunwa zamani. Mchele hupoteza ubora aina tofauti zinapochanganywa pamoja, au mavuno yakivunwa mapema au kuchelewa sana. Wateja hawapendi mchele ambao una mawe, mchanga na kadhalika. Kwa kuongezea, mchele hupata ubora duni ikiwa umekaushwa au kuhifadhiwa vibaya.
Mchele bora
Mchanganyiko wa aina tofauti za mpunga hutoa matokeo yasiyoridhisha ukiwekwa kwa mashine za kusaga. Kwaani aina ndogo ya mpunga ndiyo itakayopita vizuri,lakini ile kubwa itavunjika.Kwa hivyo unafaa kupanda kila aina kwa upande tofauti. Unafaa kuzitenganisha aina hizo tofauti waakati wa kuvuna, kupukuchua na kuhifadhi.
Mpunga ukiwa haujakomaa, utabonda ikawa unga baada ya kusafisha kwenye mashini. Lakini ukichelewa sana, mchele utatoka umevunjika wakati wa kusafisha na mashini. Unafaaa kuvuna wiki tano baada ya wimbi kuhudhuria. Wakati huo mpunga huwa na rangi ya majani hubadilika ikawa kama majani makavu ama manjano.
Uchafu kama mawe unaweza kufika kwenye mchele wakati wa kupura. Ndio sababu unahitaji sakafu safi ya kupuria nafaka. Inaweza kuwa turubai, magunia yaliyounganishwa pamoja kwa kushonwa ama sakafu iliyojengwa kwa sementi. Pura nafaka kwa mara chache na uondoe mbegu yoyote ya magugu. Kausha mpunga kwenye sakafu safi. Usianike mpunga chini kwa udongo ama kando ya barabara, kwa sababu mawe, uchafu na vijiti vinaweza kuchanganyika na mpunga kwa urahisi.
Mpunga ukiwa umekauka sana ina nyufa na huvunjika wakati wa kusaga. Kama kuna jua kali,basi kausha mpunga wako kwa masaa machache. Endelea kukausha mpunga wako katika kivuli. Pindua mpunga mara kwa mara ili mpunga wote upate kukauka kwa usawa. Ili kuona ikiwa mpunga wako umekauka vizuri, unaweza kuuma kwa meno. Ukivunjika kwa sauti kavu, basi unajua mchakato wa kukausha umekamilika.
mpunga ukihifadhiwa chini, hupata unyevu na ukungu. Mpunga ukiwekwa ndani ya magunia na kuhifadhiwa juu ya mbao zilizokauka, utakaa vizuri. Usiweke mifuko yako moja kwa moka kwenye udongo au juu ya chuma zilizo na kutu. Daima acha nafasi kati ya mifuko ndipo kuwe na hewa safi na kwa udhibiti bora wa wadudu.