Mbolea za kemikali na viuatilifu hupunguza mavuno na huharibu rutuba ya udongo vikitumiwa vibaya au kwa muda mrefu.
Kilimo hai huhimiza wakulima kuongeza mavuno kwa kutumia maliasili huku wakipunguza gharama. Tafuta eneo tambarare, lenye kivuli lililokaribu na wanapokaa mifugo. Epuka maeneo ambapo maji hukusanyika, na ambapo kuna miti ya mkuaju, mwarobaini na mbuyu kwa sababu huvutia magugu ambao hula madini asili kutoka kwenye mbolea.
Kitalu cha mbolea oza ya minyoo
Pasua magunia ya mbolea yasiyo na mashimo, kisha yashone kwa nyuzi za nailoni. Unganisha magunia na uyashone ambayo yatakuwa msingi wa kitalu cha mbolea. Kunja magunia haya ili kuunda chombo cha upana wa 3m na kina cha 1.5m huku ukishona kila mkunjo. Kata madirisha 3 ya upana wa nusu mita katika kila upande wa chombo, halufu uyafunike kwa chandarua. Madirisha hayo huruhusu hewa kuingia kwenye mbolea ili minyoo wasikufe.
Chimba ardhi iwe na mwinamo kidogo na uondoe mawe yoyote makubwa. Pima ukubwa wa mfuko ardhini. Chimba mashimo kwenye pembe zote 4 na uongeza mengine mawili kwenye pande ndefu. Weka vigingi ili kuimarisha mfuko wa mbolea.
Weka kitambaa laini au godoro nzee kwenye ardhi halafu uweke damani ya plastiki juu yake. Toboa mashimo madogo kwenye chombo kabla ya kuweka mbolea ili kuruhusu maji maji ya mbolea ya minyoo kupenyeza na kufikia ndoo iliyo chini.
Kuandaa mbolea oza ya minyoo
Weka majani makavu na nyenzo zinazoweza kuoza. Ongeza samadi ya ng‘ombe isiyo na mawe wala chembe zisizohitajika kwenye kitalu cha mbolea, na kisha umwagilie maji. Ongeza samadi mbichi juu, na ufunike kitalu kwa kitambaa kizee au gunia.
Baada ya wiki moja, ongeza minyoo kwenye mbolea na umwagilie maji mara mbili kwa siku. Funika pande zote na uchimbe shimo kwenye sehemu ya chini ili kukusanya maji maji ya mbolea ya minyoo. Hifadhi maji haya mahali palipo na kivuli. Tumia ndoo isiyo na shimo kwa kifuniko.