»Kilimo msetu cha mahindi na mbaazi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/node/17729

Muda: 

00:09:55
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

NASFAM

Kilimo msetu cha mahindi na mbaazi ni muhimu kuboresha thamani ya mahindi.

Mahindi huhitaji virutubisho vingi kutoka ardhini. Kila baada ya vuno, kiasi kadha cha virutubisho hivyo huondolewa ardhini. Baada ya kulima kwa myaka kadha, ardhi hupoteza rutuba nakadhalika, mahindi hukosa mavuno mazuri. Mahindi pia, hudumaa na huwa na rangi iliopauka yanapo kosa kupata virutubisho vya kutosha.

Mbaazi

Mbaazi husaidia kurejesha rutba ya ardhi, na pia huongeza nitrojeni ardhini kwa kuivuta kutoka hewani. Mizizi, mashina, na majani ya mimea huboresha udongo kwa kuongeza mbojo. Bora, mbaazi huendelea kunawiri hata kwenye kipindi cha kiangazi, kwasababu mizizi yao huvuta maji kuto chini kabisa ardhini.

Kilimo mseto cha mbaazi na mahindi

Kuna njia tele kadha za kulima mseto wa mbaazi na mahindi.

Kwa njia ya kwanza, tunapanda mbaazi kwa muachano wa 75 cm. Kisha, tunapanda mahindi katikati ya mimea miwili ya mbaazi.

Njia nyingine ni kwa kupanda mistari miwili ya mahindi ikifuatiwa na msatri mmoja wa mbaazi. Hakikisha kwamba kuna muachano wa 75 cm baina ya matuta, ili kusababisha uingizaji wa mwangaza wa jua wa kutosha. Matuta yanafaa kuwa juu ya 30cm. Katika misitari ya mbaazi, panda mbegu tatu nzuri kwa kila sehemu ya kupanda kwenye shimo ya kina cha 5cm. Katika mstari wa mahindi, panda mbegu moja nzuri baada kwa kila 25 cm. Hapo, mimea yatapata nafasi ya kutosha ili kuvuta virutubisho. Hakikisha kwamba unapanda mahindi na mbaazi katika siku moja ili mimea yote yaweza kupata manufaa ya mvua nyingi ya kuanza.

Njia ya tatu ni kwa kupanda mimea yote miwili kwenye tuta moja. Muachano kati ya mstari mmoja na mwengine ni 75 cm. Hapo basi, weka mbegu moja ya mahindi katika kila 25 cm. Pia, unapanda mbaazi katika kila sehemu ya tatu ya upanzi wa mahindi, na hivyo kuwa na muachano wa 75 cm kati ya mbaazi. Mwisho, panda mahindi kwenye mstari na kueka mbaazi kando ya mstari.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:10Baada ya kulima kwa myaka kadha, ardhi hupoteza rutba nakadhalika, mazao hukosa mavuno mazuri.
01:1102:25Mbaazi husaidia kurejesha rutba ya ardhi.
02:2602:37Mimea hudumaa na huwa na rangi iliopauka yanapo kosa kupata virutubisho vya nitrojeni vya kutosha.
02:3803:48Mizizi, mashina, na majani ya mbaazi huboresha udongo kwa kuongeza mbojo.
03:4904:10Mbaaza yaweza kuishi hadi myaka mitano
04:1104:52Kwa njia ya kwanza, tunapanda mbaazi kwa muachano wa 75 cm. Kisha, tunapanda mahindi katikati ya mimea miwili ya mbaazi.
04:5306:45Njia nyingine ni kwa kupanda mistari miwili ya mahindi ikifuatiwa na msatri mmoja wa mbaazi.
06:4606:58Hakikisha kwamba unapanda mahindi na mbaazi katika siku moja ili mimea yote yaweza kupata manufaa ya mvua nyingi ya kuanza.
06:5908:00Njia ya tatu ni kwa kupanda mimea yote miwili kwenye tuta moja
08:0109:55Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *