Kilimo cha papai – Mwongozo Kamili | Jinsi ya kulima papai

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=-8TI0O1mvOY

Muda: 

00:04:09
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Discover Agriculture
Loweka mbegu kwa muda wa siku 3 hadi 5, badilisha maji kila siku na panda mbegu moja kwa shimo, lakini usipande chini sana.
Panda miche kwenye chumba cha wavu ili kulinda miche dhidi ya wadudu, na funika kwa damani ya plastiki endapo mvua kubwa itanyesha.
Hamisha miche kwenye kiriba cha palstiki siku 14 baada ya kupanda. Pandikiza miche kwa muachano wa sm 10 kwa 10. Miche huwa tayari kupandikizwa siku 45 baada ya kupanda.
Dumisha unyevu mara kwa mara siku nzima na uepuke kumwagilia jioni.

Maandalizi ya Ardhi na Kupandikiza

 Udongo uliolimwa vizuri na vitalu vilivyoinuliwa husaidia kuhakikisha ukuaji wa mizizi yenye nguvu, na ukuaji wa mimea. Pia tengeneza mifereji ya maji ili kuzuia maji kutuama.
Andaa mashimo ya upanzi ya sm 10–15 yasiyo na kina kirefu na kupandikiza mimea alasiri.
Panda mpapai kwa muachano wa mita 2.5–3 kati ya safu, na mita 3m kati ya mimea, na mwagilia maji mara baada ya kupandikiza.

 Kuhakikisha mavuno ya juu

Uwekaji wa mbolea hutegemea idadi ya mimea. Changanya dawa na unyunyuzie kwa uangalifu, vaa nguo za kujikinga na osha mikono vizuri baadaye na matumizi. Nyunyizia dawa ukizingatia muelekeo wa upepo ili kuepuka kukupeperushia dawa.
Ili huhakikisha mavuno mengi, lima udongo vizuri, panda miche yenye afya, acha nafasi sahihi, dumisha unyevu mzuri kwenye udongo, epuka kutuamisha maji shambani, hakikisha matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu.
Jua wadudu na magonjwa yanayoshambulia mipapai. Tumia mitego ya wadudu kupunguza idadi ya nzi wa matunda, ondoa matunda na mimea iliyoambukizwa, na dhibiti wadudu.

Shughuli za kuvuna

Matunda huwa tayari kuvunwa miezi 6–7 baada ya kupandikizwa. Uvunaji unaweza kufanywa kati ya 9 asubuhi hadi 3 jioni ili kupunguza mtiririko wa utomvu ambao unaweza kusababisha majeraha kwenye ngozi ya tunda.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:14Kabla ya kuota na uzalishaji wa miche.
01:1502:00Maandalizi ya ardhi na kupandikiza.
02:0102:46Uwekaji wa mbolea na matumizi bora ya viuatilifu.
02:2703:18Wadudu na magonjwa ya papai na jinsi ya kuhakikishi mavuno mengi.
03:1903:40Shughuli za kuvuna na baada ya kuvuna.
03:4104:09Muhtasari.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *