Matumizi endelevu ya mbolea za kemikali na dawa za magugu huharibu udongo pamoja na viumbe hai vyenye faida. Mashine pia hulima kwa kina kirefu kwamba udongo wa juu wenye rutuba huenda chini sana, na udongo usio na rutuba huwa juu. Mashine pia husindilia udongo.
Udongo hupoteza muundo wake, huwa mgumu na mizizi ya mimea hushindwa kuupenya vizuri. Kwa hivyo, mimea hushindwa kunawiri. Kifaa cha kuvunjavunja mabonge ya udongo kinaweza kutumiwa kulima ardhi, huku kikivunja udongo kuwa wembamba zaidi.
Umuhimu wa Kifaa cha kuvunjavunja udongo
Kifaa hiki hubiringishwa shambani huku kikivunjavunja udongo katika chembe ndongo laini. Pia huchimba udongo kwa kina cha 15cm tu na hakitumii mafuta, ambalo huifanya kuwa zana nzuri kwa mazingira.
Kifaa hiki kinaweza kutumika kuandaa kitalu na shamba kwenye aina yoyote ya udongo, kwa aina yoyote ya mimea, kwa ardhi isiyolimwa au baada ya maandalizi ya kwanza ya shamba. Udongo wenye muundo mzuri una pores zaidi ya kuhifadhi maji kwa ukuaji mzuri wa mazao.
Kifaa cha kuvunjavunja mabonge ya udongo husaidia kuokoa wakati na nguvu katika udhibiti wa magugu.
Kutengeneza Kifaa cha kuvunjavunja mabonge ya udongo
Kifaa cha kuvunjavunja mabonge ya udongo hutengenezwa kutoka kwa aina yoyote ya mbao ngumu. Gogo la kipenyo cha 30cm na mita 1 kwa urefu linakatwa. Kisha gamba huondolewa ili kulipa gogo muundo wa silinda.
Kata mbao mbili zilizo na umbo la kabari kwa urefu wa 1 m pamoja na unene wa 8cm. Sehemu ya katikati ya upande mwembamba hukatwa kwa upana wa cm 2–4 na kina cha cm 5–10. Ambatisha vipande vya chuma vilivyo na ukubwa wa 5 cm kwa 3cm mwishoni mwa mbao mbili. Kisha ambatisha vyuma hivyo kwa ufito wa chuma uliyolegezwa ili kuwezesha gogo kupinduka kwa urahisi.
Kata fito mbili zilizo na urefu wa 1m na kipenyo cha 8 cm. Unganisha fito hizo katikati ili kutengeneza nira.
Maandalizi ya shamba
Kifaa cha kuvunjavunja mabonge ya udongo huvutwa mkononi na watu wawili. Mafahali wawili pia wanaweza kuvuta kifaa wakati mtu amekaa kwa kiti kilicho juu ya kifaa hiki. Vuta kifaa mara 4–6 kwa siku hiyo hiyo, huku ukipita shambani kwa njia mbadala.
Ili kuandaa shamba, endesha kifaa mara 3–5 shambani kutoka upande mmoja hadi mwingine.