Magonjwa mengi yameathiri miti kwa sababu ya mbinu duni za kupogoa ambazo husababisha michubuko au vidonda, na kuongeza uwezekano wa maambukizo.
Wakulima wanapaswa kutumia vifaa vikali vya kupogoa ambavyo vinaweza kudumu.
Kukata safi
Mikasi ya kupogoa; hizi hutumiwa kwa kuondoa ncha za matawi. Mkasi wa Lopa; hutumiwa kukata mashina madogo. Msumeno wa kupogoa; hutumiwa kukata matawi makubwa. Msumeno unafaa kuwa mkali ili uweze kukata safi kwa pembe ya digrii 45. Ufito wa kupogoa; hukata matawi yaliyo juu sana kwa pembe ya digrii 34. Mashine ya kupogoa; hukata matawi mazito na makubwa.
Sheria za jumla
Kata tawi linalokua wima kwa pembe ya digrii 45.
Kukata tawi kwa usawa kunaruhusu maji kukusanyika na hivyo kusababisha maambukizo, halafu kukata kwa mwinuko mkubwa sana husababisha vidonda vikubwa.
Usikate tawi mbali sana na shina kuu au karibu sana na shina. Hii husababisha vidonda ambavyo huchukua muda mrefu kupona.
Iwapo unakata matawi mazito, awali kata chini ya tawi na baadaye ulikate juu yalo ili kuepuka kupasuka sana.
Ua viini kwenye vifaa kupogoa ili kuzuia kuenea kwa magonjwa kutoka mti hadi mwingine.