Karanga ni mazao yenye lishe nyingi na mahitaji makubwa. Walakini, uzalishaji wake unaathiriwa na mbinu duni za kilimo ambazo wakulima hufanya.
Karanga hutoa mavuno mazuri endapo hatua na mbinu bora zitakapofuatwa, kama vile kuboresha rutuba ya udongo, kuchagua aina bora ya mbegu, na kubadilisha mimea. Badilisha mimea shambani ili kuboresha afya ya udongo na kupunguza magonjwa. Chagua udongo wa tifutifu-kichanga uliyo na rutuba, kwani karanga hazitakua vizuri katika udondo uliyo furika na maji mengi sana, na ule wa mfinyanzi. Lima na kutengeneza shamba kabla ya mvua kuanza ili uweze kupanda kwa wakati.
Kutibu mbegu
Chagua aina za mbegu zinazofaa kwa soko, na panda kwenye matuta ili kuhifadhi maji ya kutosha iwezekanavyo. Angalia kuota kwa mbegu, kwa kupanda na kumwagilia maji katika wiki mbili na uhesabu idadi ya mbegu zilizoota. Mbegu zikiota vizuri, zihamishie shambani na kuzipanda. Zikiota duni, tafuta aina mpya ya mbegu. Panda mbegu kwa muachano wa sentimita 10 hadi 15 kutegemeana na saizi ya mbegu ili kufunika shamba vizuri, kuzuia magonjwa, na kuhifadhi unyevu wa udongo kwa muda mrefu. Palilia shamba ili kuondoa magugu yote, ambayo hushindania maji, virtutbisho na mwangaza wa jua, vya mimea.