Parachichi ni mojawapo ya matunda ambayo uzalishaji wake kibiashara unaongezeka siku hadi siku. Usimamizi wa matawi ni muhimu katika kuongeza tija ya miti ya parachichi.
Ikiwa hautapogoa, miparachichi hukua sana na kutoa matawi mengi yasiyozaa matunda. Miti midogo ni salama, ni rahisi kuchuma na ni rahisi kutunzwa. Maua na matunda hukua vyema katika eneo ambalo hupokea jua moja kwa moja. Hili linaweza kupatikana kwa kudumisha miti midogo au kwa kupogoa matawi. Huku kunaruhusu mwanga wa jua kupenya ndani ya mti. Usimamizi wa matawi unahusiana na msongamano wa upandaji, yaani, kadiri msongamano wa upandaji ulivyo juu, ndivyo usimamizi wa matawi unavyokuwa mgumu.
Kuanza
Wakati wa kuanza usimamizi wa matawi, zingatia kanuni 3 za kimsungi yaani urefu wa mti usizidi asilimia 80% ya umbali ulio kati ya mstari, kwa mfano kwa umbali wa 10m ulio kati ya mstari, urefu wa mti usizidi mita 8.
Urefu wa mti unapaswa kuwa chini ya mara 2.5 upana wa njia iliyo wazi. Watu wengi huchagua njia ya mita 2 ili kuwezesha utumiaji wa mashine shambani. Urefu wa juu haupaswi kuzidi mita 5.
Punguza ukubwa wa sehemu ya mti isiyozalisha matunda . Hii hupatikana kwa kuhakikisha kwamba miti ni mifupi au kwa kupogoa matawi ili kuruhusu mwanga kupenya mti.
Muda sahihi wa kupogolea
Pogoa wakati wa miezi ya baridi kwani huku kunapunguza ukuaji wa majani mengi na hupunguza hatari ya matunda na matawi yaliyowazi kuchomwa na jua kali.
Inapowezekana, pogoa mara baada ya kuvuna ili kuupa mti muda wa kutosha wa kuzalisha matunda na kuhifadhi wanga kwa zao linalofuata.
Pogoa kwa muda ili kuzuia ukuaji wa majani mengi ambayo kushindana na maua na matunda, jambo ambalo huathiri mavuno na ubora wa matunda.