Afya ya mnyama huamua ubora na wingi wa bidhaa za wanyama zitakazozalishwa.
Kutibu wanyama ni shughuli nzuri kwa afya ya wanyama. Kwa hivyo, dawa ya eprinex hupakwa kwa mwili wa ndama wachanga, ndama jike na vile vile ng‘ombe wa maziwa na wanaonyonyesha.
Jinsi ya kunyunyizia wanyama dawa
Dawa ya eprinex inaweza kutolewa kwa kutumia mbinu ya kubana- kupima- na kumimina, au kwa kutumia kifaa maalum. Kwa hivyo, vaa glavu kila wakati unaposhughulikia dawa za kemikali. Kwa mbinu ya kubana- kupima- na kumimina, tumia chombo cha 250ml au lita 1.
Anza kwa kuingiza mrija ndani ya kifaa cha kupimia. Kisha fungua chombo na ambatisha kifaa cha kupimia juu yake. Kisha pima uzito wa mnyama ili kumtolea kipimo sahihi cha dawa. Rekebisha kifuniko cha kifaa cha kupimia ili kulinganisha kipimo cha dawa itakayotolewa na uzani wa mnyama.
Vile vile, bonyeza chombo kwa upole ili kujaza kifaa cha juu kwa kipimo kinachohitajika, na umimine dawa kwenye mgongo wa mnyama kutoka kwa bega mpaka mkia hadi kipimo kamili kitakapotolewa. Tenganisha kifaa cha kupimia na chombo kila baada ya matumizi, na kisha funika chombo kwa hifadhi ifaayo. Hata hivyo, tumia kifaa maalum cha kunyunyizia dawa kwa vyombo vya lita 2.5, lita 5 na lita 20.
Weka chemchemi kwenye mrija, na ambatisha mirija kwenye kifaa cha kunyunyizia dawa na ukirekebishe ipaswavyo.
Zaidi ya hayo, pima uzito wa mnyama, na upime kipimo cha dawa kinachofaa huku ukifuata maelekezo yaliyotolewa na mtengenezaji.
Mwishowe mimina dawa kwenye mgongo wa mnyama kutoka bega mpaka mkia hadi kipimo kamili kitakapotolewa.