Usindikaji wa mvinyo
Funika na acha mvinyo kwa siku 3 huku ukikoroga mara moja kwa siku 3. Ondoa kifuniko kisha uweke tena kifuniko na uache mvinyo kwa wiki 2 zaidi. Ondoa chachu iliharibika na baada ya wiki 2 hamishia mvinyo kwenye chombo kingiine. Angalia uzito wa mvinyo kwa kutumia kipima uzito. Pima kiwango cha kileo cha mvinyo.
Vile vile, ongeza kidonge cha campden kama kihifadhi cha mvinyo na ukoroge ili kuyeyusha kidonge. Acha mvinyo kwa usiku mmoja na ongeza sukari ili kuboresha ladha ya mvinyo.
Onja ladha ya mvinyo na ujaze kwenye chupa. Weka lebo kwenye chupa hizo kwa asilimia ya kileo cha mvinyo.