Ubora wa mboji huamua kiwango cha uzalishaji bora, na kiasi cha mavuno shambani.
Utengenezaji wa mboji ya minyoo huhusisha kutumia aina fulani za minyoo ambayo husaidia katika uozo wa nyenzo za kikaboni kwa matokeo bora. Hata hivyo, nyenzo zozote za kikaboni zinazopatikana zinaweza kutumika kwa kutengeneza mbolea ya minyoo.
Maandalizi ya mbolea minyoo
Kitalu cha mbolea ya minyoo hutayarishwa kwa ukubwa wa mita 1 x 5 na kujazwa na nyenzo za kikaboni. Kitalu humwagiliwa na maji ili kuweka unyevu.
Kilo 1 ya minyoo huongezwa katika kila kitalu ili kuozesha nyenzo za kikaboni na hivyo kutoa mboji/mbolea.
Baada ya kuongeza minyoo, kitalu hufunikwa, na kuhakikisha uingizaji mzuri wa hewa. Hata hivyo, epuka kufunika kwa kutumia damani za plastiki ili kudhibiti ongezeko la joto na gesi. Epuka nyenzo ambazo huvutia mchwa, na kagua kiwango cha unyevu mara kwa mara.
Kuvuna ya mboji/ mbolea minyoo
Mbolea ya minyoo huwa tayari kuvunwa baada ya mwezi 1 na uvunaji huanzia juu ya kitalu. Chekecha ili kutenganisha minyoo fundu na nyenzo ambzao haziozi. Rudisha mabaki kwenye kitalu
Uhifadhi na matumizi ya mbolea ya minyoo
Tumia mbolea mara tu baada ya kuvuna, au uihifadhi ili kutumika kama mbolea baada ya kukaushwa. Kiasi cha mbolea kinachowekwa kwenye mmea hutegemea aina ya mmea na nyenzo zilizotumika, na hutumiwa vyema kama mchanganyiko wa kukuza miche.