Kung‘oa magugu moja baada ya nyingine ni kazi ngumu ambayo wakulima huchukia zaidi. Kuna njia nyingi za asili za kuondoa magugu shambani.
Viua magugu vya kawaida huwa na kemikali hatari ambazo huathiri mazingira pamoja namazao. Kemikali hizi pia zinaweza kukaa kwenye udongo kwa muda wa mwaka mmoja. Kemikali hizi za pia ni hatari kwa binadamu na wanyama. Kuna dawa rahisi za asili za kuua magugu ambazozinaweza kutengenezwa nyumbani. Dawa hizi za asili zinaweza kusaidia kuondoa magugu kwa njia asili.
Njia za kuua magugu
Njia ya kwanza inahusisha kuchanganya sehemu mbili za siki na sehemu moja ya maji kwenye chupa ya kunyunyizia dawa, na kuongeza matone machache ya sabuni. Mchanganyiko hunyunyizwa kwenye magugu asubuhi.
Njia ya pili inahusisha kuchanganya vijiko vitatu vya chumvi na maji moto. Mchanganyiko wa chumvi huua magugu kwa kusababisha upungufu wa maji katika mmea, lakini pia huboresha udongo.