Kuna njia kadhaa ambazo mtu anaweza kuanzisha bustani za jikoni kwenye nafasi ndogo. Bustani hizi ni pamoja na bustani ya koni, bustani ya ghorofa nyingi, bustani ya matairi, bustani nyevu na bustani ya matone.
Bustani ya jikoni ya matairi imekuwa njia maarufu katika mbinu za kilimo. Bustani hizo zinaweza kutengenezwa kwa miundo tofauti, urefu tofauti, ukubwa tofauti na rangi tofauti kwa kutumia vifaa vya kienyeji vinavyopatikana nchini. Bustani ya matairi haipaswi kujengwa chini ya kivuli na eneo lililochaguliwa linapaswa kuwa tambarare
Kutengeneza bustani ya matairi
Kata sehemu ya juu ya tairi ili kukupa nafasi zaidi, na upake rangi tairi. Kata damani ya plastiki na uitandaze katikati ya tairi kabla ya kuweka udongo.
Mimina udongo uliochanganywa na mbolea kwenye tairi kwa uwiano wa 1: 1, na ujaze hadi ukingo wa tairi . Mwagilia maji, na kisha panda miche unayotaka. Bustani ya tairi moja ni nzuri kwa upandaji wa mboga na matunda rahisi kama vile mizabibu. Bustani ya matairi mawili ni ya mazao ya mizizi.
Bustani ya matairi ya ghorofa
Anza na kuchuka vipimo vya sehemu utakapoanzisha bustani. Weka ufito thabiti katikati mwa sehemu uliyopima. Hakikisha kwamba ufito uko thabiti sana kushikilia idadi ya matairi ambayo yana udongo. Weka nguzo kwenye saruji ili kuimarisha ufito.
Panga matairi yako kutoka chini, tairi kubwa inapaswa kuwa chini. Pima futi 2 kutoka ardhini kisha weka jukwaa linalofuata kulingana na mboga unayotaka kulima. Toa nafasi ya kutosha kati ya matairi ili kuruhusu mazao kukua vyema.
Unaweza kupanda mboga mbalimbali katika kila tairi.