»Jinsi ya Kutambua na Kudhibiti Bungua mweusi wa shina la mikahawa«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=FueE7jIx5HQ

Muda: 

00:04:21
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Uganda Coffee Platform Extension Videos

Kwa kuwa ni zao linalohitajika sana kutokana na umuhimu wake, ukuzaji na uzalishaji wa kahawa huathiriwa na mambo mbalimbali ambayo ni pamoja na bungua mweusi wa mashina ya mikahawa na rutuba duni ya udongo.

Bungua mweusi ni mdudu mdogo mweusi unaong‘aa ambao una urefu wa 1–2 mm, na umbo la mviringo. Mdudu huo hukaa kwenye matawi ya mikahawa. Bungua jike hujipenyeza kwenye tawi na kuchimba mashimo ya ukubwa wa pini.

Kutambua wadudu

Uwepo wa wadudu hutambuliwa kwa urahisi na dalili kama vile majani kugeuka njano, mashimo madogo chini ya matawi, vumbi nyeupe kwa mashimo ya kuingilia, na matawi dhaifu.

Dalili zingine ni kunyauka, majani na matawi kubadilika rangi kuwa meusi kutoka kwenye shimo la kuingilia na kuelekea juu ya tawi lililoathirika.

Udhibiti wa wadudu

Kuna haja la ukaguzi wa shamba wa kila siku ambao husaidia katika kutambua wadudu, na hivyo kuwadhibiti mapema. Ondoa sehemu za mmea zilizoathiriwa na uzichome ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa.

Ongeza mbolea shambani ili kustawisha mimea, mwagilia maji na punguza kivuli shambani.

Epuka kupanda miti ambayo huhimiza bungua mweusi wa mashina ya mikahawa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:35Bungua mweusi wa mashina ni mdudu mdogo mweusi unaong‘aa ambao una urefu wa 1–2 mm, na umbo la mviringo.
00:3600:49Mdudu huo hukaa kwenye matawi. Bungua jike hujipenyeza kwenye tawi na kuchimba mashimo ya ukubwa wa pini.
00:5001:12Wakishaingia, wanachimba mashimo kwenye matawi machanga ya kahawa na hivyo kuyawaua.
01:1301:27Dalili za shambulio ni pamoja na majani kugeuka njano, mashimo madogo chini ya matawi.
01:2801:46Uwepo wa vumbi nyeupe kwa mashimo ya kuingilia, na matawi dhaifu
01:4702:07Dalili zingine ni kunyauka, majani na matawi kubadilika rangi kuwa meusi kutoka kwenye shimo la kuingilia na kuelekea juu ya tawi.
02:0802:38Ili kudhibiti ugonjwa, fanya ukaguzi wa shamba kila siku, ondoa sehemu zilizoathirika na uzichome.
02:3904:18Ongeza mbolea shambani ili kustawisha mimea, mwagilia maji na punguza kivuli shambani.
04:1904:21Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *