Kupogoa ni kuondoa matawi yasiyohitajika kutoka kwa mti. Ni hatua muhimu katika usimamizi wa miti ya matunda.
Kupogoa hukuruhusu kubebesha mtufaa mara kadhaa. Unaweza kuunganisha hadi aina 5 za tufaha kwenye mti mmoja. Ili kufanya hivyo, himiza ukuaji wa matawi chini, jambo ambalo hufanywa kwa kupogoa mti hadi inchi 15 kutoka ardhini. Hii huhimiza mmea kutoa machipukizi ambayo kisha hukunjwa. Kuunganisha aina nyingi kwenye mti mmoja huruhusu uvunaji wa matunda kwa muda mrefu.
Vidokezo vya kuunganisha
Kunja matawi ipaswavyo kwa kutumia vijiti. Kukunja matawi huhakikisha kwamba mti hupata mwanga wa kutosha, na hivyo kuhakikisha mavuno mengi. Pia kunahakikisha kwamba hewa na mwanga wa jua kupenya vizuri, na hivyo basi kupunguza matukio ya magonjwa.
Baada kuunganisha miche acha muda wa kati ya wiki 3 hadi 6 ili kuwezesha mche-shina na kikonyo kushikamana vizuri. Vipande hivyo vinaweza kuunganishwa kwa kutumia kamba ya nailoni.
Baada ya kuunganisha, unapaswa kupogoa mche. Baada ya wiki 6 hadi 8, kata sehemu ya chini ya mche-shina na sehemu ya juu ya kikonyo. Katika mwaka wa kwanza, usiruhusu kikoyo kuzaa matunda kwani uzani ulioongezwa na matunda yaliyozaliwa unaweza kuvunja muungano.
Linda muungano dhidi ya panya, wadudu na magonjwa. Pia linda shina la mti dhidi ya wadudu na magonjwa.
Tolea mimea yako mbolea yenye virutubisho vyote muhimu ambavyo vinahitajika. Virutubisho vya jumla ni pamoja na nitrojeni, fosforasi, potasiamu, magnesiamu, salfa na kalsiamu.