Jinsi ya kukuza mtama

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=E1FQ3QcWHR4

Muda: 

00:10:16
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Agri Farming
Mtama ni kundi la nyasi ndogo zenye mbegu zinazokuzwa ulimwenguni kote kama zao la nafaka kwa chakula cha binadamu na malisho ya mifugo.
Mtama huchukua jukumu muhimu katika kuzuia na kuponya maradhi kadhaa. Mtama una virutubishi vingi vilivyoboreshwa kiasili. Mtama ni chanzo kikubwa cha fumuele, madini kama vile magnesiamu, fosforasi, chuma, kalsiamu, zinki na potasiamu. Mtama huhitaji halijoto ya joto ili kuota na kukua vizuri na huathiriwa na baridi. Joto bora la udongo kwa ajili ya uotaji mzuri wa mbegu ni kati ya nyuzi joto 68 hadi 86.

Mahitaji ya udongo

Mtama huzaa vizuri kwenye udongo tifutifu usiotuamisha maji. Mtama huenezwa na mbegu au nafaka. 
Nitrojeni kwa kawaida ni kirutubisho muhimu zaidi katika uzalishaji wa mtama. Viwango vya nitrojeni vitakavyohitajika hutegemea mavuno, ukuaji wa mmea, pamoja na historia ya upandaji wa mazao.  Nitrojeni nyingi sana kupita kiasi huathiri ukuaji wa mtama.

Aina mbalimbali

Mtama huhitaji joto la wastani la angalau nyuzi joto 25 ili kutoa mavuno mengi katika mwaka husika. Wadudu na magonjwa si changamoto kubwa kwenye mtama lakini ndege ni tishio kuu.
Mtama aina ya pearl ni chanzo kikubwa cha fosforasi ambayo husaidia katika muundo wa seli za mwili. Mtama aina ya wimbi una kalsiamu na protini nyingi na kiwango kizuri cha madini ya chuma na madini mengine.

Udhibiti wa wadudu

Panzi ni wadudu waharibifu zaidi kwenye mtama. Tumia dawa za kuua wadudu ili kudhibiti panzi. Viwavijeshi pia hushambulia mtama lakini bado vianaweza kudhibitiwa kwa njia ya kutumia dawa.
Mtama huwa tayari kuvunwa wakati mbeguzilizo kwenye sehemu ya juu ya gunzi zimekomaa. Mbegu zilizo katika sehemu chini ya gunzi lazima iwe zimepoteza rangi yazo ya kijani kibichi. Kwa wakati huu, majani na mabua bado yainaweza kuwa rangi kijani kibichi.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:45Mtama ni kundi la nyasi ndogo zenye mbegu zinazokuzwa ulimwenguni kote kama zao la nafaka kwa chakula cha binadamu na malisho ya mifugo.
00:4601:30 Mtama huhitaji halijoto ya joto ili kuota na kukua vizuri na huathiriwa na baridi.
01:3102:20Mtama huzaa vizuri kwenye udongo tifutifu usiotuamisha maji.
02:2103:00Mtama huenezwa na mbegu au nafaka.
03:0104:00Nitrojeni kwa kawaida ni kirutubisho muhimu zaidi katika uzalishaji wa mtama. Nitrojeni nyingi sana kupita kiasi huathiri ukuaji wa mtama.
04:0105:00Mtama huhitaji joto la wastani la angalau nyuzi joto 25 ili kutoa mavuno mengi katika mwaka husika.
05:0106:10Wadudu na magonjwa si changamoto kubwa kwenye mtama lakini ndege ni tishio kuu.
06:1107:00Mtama ambao ni maarufu kusini mwa India unaweza kukuzwa katika hali ya hewa ya joto
07:0108:10Magonjwa ni tatizo kwenye mtama lakini yanaweza kuzuiwa kwa kutumia mbegu zilizobibiwa, na pia kufanya mzunguko wa mazao
08:1109:11Mtama huwa tayari kuvunwa wakati mbeguzilizo kwenye sehemu ya juu ya gunzi zimekomaa.
09:1210:16Panya na ndege wanaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa mtama. Udhibiti wa mara kwa unahitajika.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *