Kaya nyingi hufuga kuku, lakini changamoto kubwa inayowakabili wafugaji ni magonjwa.
Kuepuka magonjwa ni muhimu sana katika ufugaji wa kuku. Ni bora kutekeleza hatua za kuzia na kudhibiti uenezaji wa magonjwa. Magonjwa husababisha hasara za kiuchumi katika ufugaji wa kuku. Hasara ni pamoja na vifo vya ndege, uzalishaji duni, na gharama za udhibiti wa magonjwa.
Vidokezo vya kuzuia magonjwa
Muundo wa banda la kuku ni muhimu katika kuzuia magonjwa. Banda linapaswa kujengwa kwa namna ambayo ndege hawagusi kinyesi chao. Jenga banda lenye sakafu iliyoinuliwa ili kuruhusu kinyesi cha ndege huanguka chini na kuondolewa wakati wa kusafisha.
Tekeleza mbinu ya ufugaji wa kuku ambapo kundi fulani la vifaranga huletwa, kutunzwa na woto huuzwa, kisha kundi lingine huleetwa. Osha vihori vya maji na chakula. Pia punguza idadi ya wageni kwenye shamba.
Fuataa ratiba ya kuchanja ndege dhidi ya magonjwa ya virusi.
Dumisha usafi wa vihori vya maji na chakula. Epuka kuchafua malisho na maji kwa kutumia vihori maalum.
Chunguza ndege mara kwa mara ili kutambua magonjwa mapema. Kabla ya kuanza ufugaji wa kuku, ni muhimu uwe na mafunzo ya kutambua na kutibu magonjwa.