Kwa kuwa ni mojawapo ya mambo yanayoathiri ufugaji wa wanyama, afya ya mnyama huamua ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kutoka kwa wanyama.
Dawa ya prolyflex husaidia ng’ombe kustahimili magonjwa ya kupumua. Dawa hii huuzwa kama unga mkavu ambao huchanganywa na maji safi ili kuunda myeyusho. Kiasi cha maji kinachotumiwa kuchanganya dawa hutegemea ukolezi unaohitajika.
Jinsi ya kutolea mnyama dawa
Kwanza, rejelea maandishi yaliyochapwa kwenye chupa ya bidhaa kwa maelezo mahususi. Tumia sindano mpya na bomba la sindano, chota maji safi na uyahamishie kwenye chupa ya polyflex. Kisha changanya vizuri na andika tarehe na ukolezi wa dawa kwenye chupa.
Vile vile, mfunge mnyama kabla ya kumdunga kwa ajili ya usalama na ustawi wa mnyama. Unapochagua sindano inayofaa kutumiwa, pima uzani wa mnyama na kisha upime kipimo sahihi cha dawa ya polyflex. Tafuta mahali pa kudunga sindano na kwa hili, kutumia mfumo wa pembetatu kwenye shingo ndiyo njia inayopendelewa zaidi. Eneo hilo hupatikana chini ya upande wa shingo mbele ya bega la mnyama. Epuka kudunga mshipa wa shingo.
Mara baada ya kutambua eneo hilo, ingiza sindano kwenye msuli na sukuma dawa ndani. Kisha ondoa sindano na tumia sindano mpya kwa kila mnyama ili kuepuka uchafuzi wa dawa.
Zaidi ya hayo, weka alama kwenye wanyama waliotibiwa na uwaweke kwenye zizi hadi muda kadhaa. Hifadhi dawa iliyosalia kwa nyuzi joto 30 hadi 40 ili kudumisha ukolezi wake kwa miezi 3.
Hatimaye, tikisa vizuri ili kuchanganya dawa iwapo unapotumia chanjo, na fuata maelekezo yaliyoandikwa kwenye chupa, pamoja na kuasiliana na daktari wa mifugo.