Kwa uchaguzi sahihi wa eneo la mabwawa, pamoja na kuhakikisha uzingatiaji unaofaa, wakulima wanaweza kufaidika zaidi katika ufugaji wa samaki. Hata hivyo, uchaguzi duni husababisha changamoto kadhaa.
Vyanzo vya maji vya kawaida kwa mabwawa ya samaki ni pamoj na mito midogo, visima na maji kutoka kwenye paa. Funga ukuta wa bwawa ili kuzuia upotezaji wa maji, au tengeneza mabwawa ya zege.
Uchaguzi wa eneo
Chagua eneo lenye mwinuko wa ardhi uliyo teremka ili kuwezesha maji kutiririka ndani na nje ya bwawa.
Daima epuka maeneo tambarare kwa sababu haya huathiriwa na mafuriko wakati wa mvua kubwa.
Epuka maeneo yenye mwinuko sana, kwani yanahitaji kazi nyingi za ujenzi, na pia kuta zinaweza kuanguka wakati wa mvua kubwa.
Chagua eneo lisilo na mawe makubwa.
Udongo usiwe na kokoto nyingi,changarawe wala mchanga kwa kuwa vinahimiza upotevu wa maji.
Pia epuka udongo wa mfinyanzi kwa vile udongo hutoa nyufa ambazo husababisha upotevu wa maji.
Epuka maeneo yenye miti mikubwa ambayo inaweza kuenea hadi kwenye mabwawa na pia mizizi inaweza kuacha mapengo baada ya kuoza, ambazo hupitisha maji.
Epuka maeneo yenye mchwa kwa vile pia hutengeneza mashimo kwenye udongo na hivyo kupitisha maji.
Mambo ya kuzingatia wakati wa kuchagua eneo
Zingatia usalama, soko na ufikiaji wa shamba ili wateja waweze kupata bidhaa kwa urahisi.
Pia zingatia gharama za kazi kwa ajili ya kupanga vizuri.