Mbinu ya banda kitalu ni aina ya kilimo ambapo mimea hupandwa katika muundo uliofunikwa na damani ya plastiki juu yake.
Mbinu hii ya kilimo imepata umaarufu nchini Kenya kwa kuwa ni kitega uchumi, na pia huwezesha utekelezaji rahisi wa mbinu za kilimo. Mazao ya chakula yanayolimwa kwenye banda kitalu ni pamoja na; matango, sukumawiki, nyanya, pilipili hoho, na mchicha. Nyanya ni zao kuu linalopandwa katika banda kitalu, kwani hustawi vizuri katika kitalu hicho.
Kukuza nyanya
Nyanya hukua vizuri kwenye vitalu vilivyoinuliwa na hali bora ya udongo ambayo. Udongo wenye rutuba ni muhimu kwani huisaidia katika ukuaji bora wa nyanya, na hivyo mmea hukua hadi mita mbili kwa urefu.
Nyanya pia huhitaji nafasi ya kutosha ili kuwezesha utendaji mzuri wa mbinu za usimamizi. Umbali unapaswa kuwa cm 30 kati ya vitalu.
Maandalizi ya kitalu
Udongo wa kitalu hulimwa, na kuchanganywa na samadi. Kisha subiri kwa muda wa wiki mbili ili samadi ichanganyke vizuri na udongo, pamoja na maji. Baada ya wiki mbili, mashimo ya kupandia miche huchimbwa na mbolea ndani yake na kuchanganywa vizuri kwenye udongo.
Kumwagilia kwa kawaida hufanywa asubuhi, kwani mbegu zilizopandwa zinatarajiwa kuanza kuota baada ya siku nane, na kumwagilia kunapaswa kuendelea kwa wiki moja au mbili kabla ya kupanda.
Digging of beds is first done and soil is then mixed with manure after which one waits for two weeks in order for manure to be ready and mixed with the soil as well as water. After two weeks are over, holes for planting the seedlings are dug and fertilizer is put in them and mixed well in the soil.
Watering is usually done in the morning hours as the planted seeds are expected to start sprouting after eight days and watering should continue for a week or two before transplanting is done.
Utunzaji bora
Kupandikiza kwa kawaida hufanyika wiki moja au mbili baada ya mbegu kuota ili kuepuka kuharibu miche.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa banda kitalu halivuji. Kisha mabomba yenye mashimo huwekwa kwenye vitalu ili kumwagilia mimea maji. Mabomba hutumiwa ili kuzuia athari ya kunyunyiza maji wakati wa kumwagilia.