Nyanya ni mojawapo ya mboga zinazotumiwa sana ulimwenguni kote, lakini uzalishaji huathiriwa na magonjwa mengi.
Haijalishi mpango wako wa mbolea ni bora kiasi gani, ubora wa udongo, usimamizi wa maji na aina za nyanya, ikiwa utashindwa kudhibiti magonjwa kwenye shamba lako, mavuno yako yataathiriwa. Magonjwa hutokea tu iwapo kuna mazingira mazuri ya ugonjwa huo kustawi, kwa mfano majani yenye unyevunyevu, aina zisizo na upinzani dhidi ya magonjwa, na viini hatari kama vile bakteria waharibifu, fangasi, virusi au minyoo fundo.
Utambuzi na mapendekezo
Daima hakikisha kwamba unatambua hali ya magonjwa kabla ya kupendekeza matibabu. Kujua jinsi ya kutambua ni muhimu ili kufanya maamuzi sahihi. Wakati wa uchunguzi, angalia majani na shina ili kutambua aina yoyote ya kasoro kama vile madoa, kubadilika rangi, ukungu, kuoza kwenye majani, na shina, au majani yaliyopinda.
Wakati ishara yoyote inapotambuliwa, inaonyesha kuwa kuna kitu kibaya kinachotokea, na kabla hakijaenea, unahitaji kukidhibiti. Magonjwa ni bora kudhibitiwa kwa kuyazuia badala ya kutibiwa.
Magonjwa ya kawaida ya nyanya ni mnyauko, ukungu, madoa kwenye majani au mashina, n.k.
Dalili zinapotambuliwa, mikakati ya kufuata ni; kumwagilia asubuhi tu, kuondoa majani ya mmea ulioambukizwa, kuondoa au kupunguza magugu, kung‘oa majani mazee, na kunyunyizia dawa za kuua kuvu.