Samadi ya kuku huongeza ukuaji wa viazi, na hilo linahitaji hatua rahisi na hivyo kuongeza mapato ya shamba.
Hata hivyo, unapopanda viazi unapaswa kuepuka kutumia samadi mbichi ya kuku kwani ina unyevu mwingi. Pia panda viazi haraka iwezekanavyo ili kuzuia machipukizi kukatika. Kuna wadudu mbalimbali wanaotokana na kutumia samadi ya kuku, na hawa ni pamoja na minyoo nyeupe na sota. Hata hivyo wadudu hawa wanaweza kudhibitiwa kiasili kwa kunyunyizia mchanganyiko wa sabuni, na viuatilifu vinavyopendekezwa.
Kilimo cha viazi
Anza kwa kuhifadhi viazi kwenye chumba chenye giza kwa muda wa wiki 3 ili viweze kuota. Chimba mashimo kwa umbali wa mita 1, kina cha cm 30–50, katika safu na umbali wa cm 60– 70 kutoka mmea mmoja hadi mwingine.
Kusanya samadi ya kuku wenye umri kati ya wiki 1– 2, kwani hii ina unyevu kidogo na kisha iweke kwenye mashimo.
Kisha funika miche ya viazi kwa udongo kidogo ili kuruhusu kuota kwa urahisi.
Daima dhibiti wadudu kwa kunyunyizia mchanganyiko wa sabuni, na viuatilifu vinavyopendekezwa.
Mwishowe, dawa za kuua wadudu zinapaswa kutumika mara moja kila baada ya wiki 2 hadi kuvuna, na pia mwagilia shamba ili kuzuia mimea kukauka.