»Hatua za kukuza malisho ya ngano/ shayiri kwa njia ya mchanganyiko wenye rutuba bila udongo (hydroponics) barani Afrika«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=f1OYag_LUvA

Muda: 

00:05:55
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

GRANDEUR AFRICA

Kilimo cha hydroponic kinahusisha upandaji wa mimea bila kutumia udongo. Aina hii ya kilimo haihusishi mbinu nyingi, na inaweza kupokelewa kwa urahisi na wakulima.

Kuna nyenzo za msingi zinazohitajika ambazo ni pamoja na mbegu safi, maji safi na trei ya alumini ili kuzuia kutu. Mbegu za shayiri huanza kuota baada ya siku moja. Hata hivyo, wakati wa kuvuna shayiri zingatia aina ya mnyama utakaomlisha. kwa mfano, kwa nguruwe na sungura vuna shayiri katika siku 6 na kwa ng‘ombe, mbuzi na kondoo vuna katika siku 8.

Hatua za kupanda

Kwanza pima uzito wa mbegu ambazo zinaweza kutoshea kwenye trei na uziloweke ndani ya maji kwa muda usiozidi saa 4.

Kisha ondoa maji na ufunike mbegu ndani ya ndoo iliyo na matundu juu ya mfuniko ili kuwezesha uingizaji mzuri wa hewa ya oksijeni, na hivyo kuhimiza uota.

Mwaga kiganja cha maji kwenye mbugu kila baada ya saa 12 ili kudumisha unyevu, tikisa mbegu ili zichanganyike vizuri. Kisha panda mbegu kwenye trei safi na uzitandaze kwa usawa ukitumia mkono ili kuhimiza uotaji sawa.

Hakikisha umeacha nafasi ndogo kwenye ncha moja ya trei ili kuepusha mizizi ya malisho kuziba matundu ya trei. Weka trei kwenye eneo la kukuzia malisho, huku upande wenye matundu ukielekea chini.

Mwagilia mbegu za shayiri angalau mara 3 kwa siku, na vuna kulingana na aina ya mnyama utakaomlisha.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:07Nyenzo za msingi zinazohitajika ni pamoja na mbegu safi, maji safi na trei ya alumini.
01:0801:48Pima uzito wa mbegu na uziloweke ndani ya maji kwa muda usiozidi saa 4.
01:4902:14Kisha ondoa maji na ufunike mbegu ndani ya ndoo iliyo na matundu juu ya mfuniko.
02:1503:37Loanisha mbegu kila baada ya masaa 12, mizizi ya mbegu huanza kuota baada ya siku moja.
03:3803:59Panda mbegu kwenye trei safi na uzitandaze kwa usawa ukitumia mkono
04:0004:34Weka trei kwenye eneo la kukuzia malisho, huku upande wenye matundu ukielekea chini.
04:3505:22Mwagilia mbegu za shayiri angalau mara 3 kwa siku, na vuna katika siku ya 4.
05:2305:36Kwa malisho ya nguruwe na sungura, vuna shayiri katika siku 6 na kwa ng‘ombe, mbuzi na kondoo vuna katika siku 8.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *