Muhogo ni zao muhimu katika jamii nyingi barani Afrika, lakini mavuno yake kwa ujumla ni madogo. Baadhi ya hatua zinaweza kufuatwa wakati wa ukuzaji wa muhogo ili kuongeza mavuno.
Ili kupata mavuno mengi ya muhogo, chagua eneo linalofaa ambalo halipo kwenye mteremko, halina maji mengi, mawe au lenye kina kifupi sana. Andaa shamba kwa kufyeka na kata vichaka, au kulima iwapo vichaka ni vingi sana. Unaweza pia kufyeka nyasi na magugu ya kudumu na kisha usubiri kwa wiki 2 hadi mimea itakapokufa. Weka dawa ya glyphosate kwenye nyasi zinazochipuka tena. Glyphosate pia inaweza kutumika kwenye shamba lenye nyasi zisizozidi mita moja kwa urefu.
Maandalizi ya ardhi
Kutayarisha shamba kwa ukuzaji wa mihogo, lima ardhi. Gharama za kulima ni kubwa lakini husababisha mavuno mengi. Kulima huongeza mavuno kwa angalau tani 5 kwa ekari. Kutengeneza matuta pia kunaweza kufanywa kwa sababu huongeza mavuno kwa angalau tani 4 kwa ekari. Huku kunapendekezwa iwapo udongo ni wa mfinyanzi mwingi au unapopanga kuvuna wakati wa kiangazi. Baada ya maandalizi ya ardhi, panda mihogo.
Kupanda na kudhibiti magugu
Panda muhogo wakati udongo unapokuwa na unyevu. Panda kwa umbali wa mita 1 kati ya safu na mita 0.8 ndani ya safu, kisha weka dawa ya kuua magugu baada ya kuibuka.
Wakati magugu yanapofunika asilimia 3o% ya shamba au mihogo inapofikia hatua ya majani 4 hadi 6, kutumia dawa za kuua magugu, palizi kwa mitambo au kwa mikono. Unapotumia dawa ya kuua magugu, weka kizuizi kwenye kinyunyizio ili kuzuia dawa kugusa sehemu za kijani za muhogo. Usitumie dawa ile ile ya kuua magugu mwaka baada ya mwaka, kwani hii inaweza kusababisha ukuaji wa magugu sugu.