»Jinsi ya kutengeneza mbolea ya minyoo shambani»

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=2-fSmPRIBEI&list=RDCMUCGLRDV5V1lCefotYPFCaG4g&index=6

Muda: 

00:03:38
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

East-West Seed Knowledge Transfer

Ubora wa mboji huamua kiwango cha uzalishaji bora, na kiasi cha mavuno shambani.

Utengenezaji wa mboji ya minyoo huhusisha kutumia aina fulani za minyoo ambayo husaidia katika uozo wa nyenzo za kikaboni kwa matokeo bora. Hata hivyo, nyenzo zozote za kikaboni zinazopatikana zinaweza kutumika kwa kutengeneza mbolea ya minyoo.

Maandalizi ya mbolea minyoo

Kitalu cha mbolea ya minyoo hutayarishwa kwa ukubwa wa mita 1 x 5 na kujazwa na nyenzo za kikaboni. Kitalu humwagiliwa na maji ili kuweka unyevu.

Kilo 1 ya minyoo huongezwa katika kila kitalu ili kuozesha nyenzo za kikaboni na hivyo kutoa mboji/mbolea.

Baada ya kuongeza minyoo, kitalu hufunikwa, na kuhakikisha uingizaji mzuri wa hewa. Hata hivyo, epuka kufunika kwa kutumia damani za plastiki ili kudhibiti ongezeko la joto na gesi. Epuka nyenzo ambazo huvutia mchwa, na kagua kiwango cha unyevu mara kwa mara.

Kuvuna ya mboji/ mbolea minyoo

Mbolea ya minyoo huwa tayari kuvunwa baada ya mwezi 1 na uvunaji huanzia juu ya kitalu. Chekecha ili kutenganisha minyoo fundu na nyenzo ambzao haziozi. Rudisha mabaki kwenye kitalu

Uhifadhi na matumizi ya mbolea ya minyoo

Tumia mbolea mara tu baada ya kuvuna, au uihifadhi ili kutumika kama mbolea baada ya kukaushwa. Kiasi cha mbolea kinachowekwa kwenye mmea hutegemea aina ya mmea na nyenzo zilizotumika, na hutumiwa vyema kama mchanganyiko wa kukuza miche.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:16Utengenezaji wa mboji ya minyoo huhusisha kutumia aina fulani za minyoo ambayo husaidia katika uozo
00:1700:22Nyenzo zozote za kikaboni zinazopatikana zinaweza kutumika
00:2300:45Tayarisha kitalu cha mbolea minyoo, na ongeza nyenzo za kikaboni
00:4600:58Kitalu humwagiliwa na maji mara kwa mara. Ongeza Kilo 1 ya minyoo fundu.
00:5901:10Minyoo hula nyenzo za kikaboni, na hivyo huzalisha mbolea.
01:1101:27Funika kitalu, himiza uingizaji hewa mzuri na epuka kutumia damani za plastiki.
01:2801:38Unaweza kutumia chombo huku ukiweka nyenzo kama vile taka za jikoni.
01:3902:06Epuka nyenzo ambazo huvutia mchwa, na kagua kiwango cha unyevu mara kwa mara.
02:0702:24Vuna mbolea minyoo kuanzia juu, kwani huwa tayari baada ya mwezi 1.
02:2502:46Chekecha mbolea minyoo na uitumie mara moja au uihifadhi.
02:4702:50Kausha mbolea minyoo kabla ya kuihifadhi.
02:5102:55Mbolea minyoo imekithiri virutubisho vinavyohitajika kwa mmea.
02:5603:09Kiasi cha mbolea kinachowekwa kwenye mmea hutegemea aina ya mmea na nyenzo zilizotumika.
03:1003:27Mbolea minyoo inaweza kuchanganywa ili kunawirisha miche, na hutumiwa vyema ikiwekwa kando ya mmea.
03:2803:38Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *