Muhogo ni chakula kikuu barani Afrika na ubora wa vipandikizi vyake huathiri mavuno, na pia husababisha maambukizi ya wadudu na magonjwa. Kwa hivyo unahitaji kuwa muangalifu wakati wa kuchagua vipandikizi vya mihogo.
Vipandikizi vya mihogo vinapaswa kuchaguliwa kwa uangalifu. Vinapaswa kuwa na afya, vimekomaa vizuri, na urefu wa 30cm. Vipandikizi vinapaswa kuwa vinene ili kuhifadhi virutubisho vya kutosha na viwe na angalau vifundo 5. Mizizi na mashina kawaida hukua kutoka kwenye vifundo. Mimea ambayo vipandikizi hukatwa inapaswa kuwa kati ya miezi 6 hadi 18. Iwapo mmea una miezi 6, huwa laini, na machipukizi (vijicho) mengi ya kijani kibichi kumbe tunahitaji mashina magumu. Mashina lazima yasiwe na wadudu wala magonjwa ili mmea uweze kustawi vyema. Kwa hivyo kuna haja la kutibu mashina kabla ya kupanda.