Mmea wa kitunguu utakua mahali popote.Unaweza kutupa kitunguu kwenye udongo wowote na hatimaye kitaota mizizi na kikaanza kukua.
Jambo la kwanza muhimu ni wakati wa kupanda. Vitunguu vina hatua mbili za ukuaji. Kuna hatua ya kutoa majani na kisha hatua ya kutoa vitunguu. Katika hatua ya kutoa majani, hakikisha kwamba mmea unatoa majani mengi iwezekanavyo. Kila majani lililo kwenye mmea litawakilisha pete kwenye kitunguu na hiyo kadri majani yanavyoongezeka ndivyo vitunguu vinavyokuwa vikubwa. Kupanda mapema ni muhimu kwani huku kunawezesha mimea kupata majani mengi iwezekanavyo.
Kupanda na kumwagilia
Bomba la kumwagilia maji kwa njia ya matone unaweza kuwekwa shambani kila baada ya futi mbili ili kumwagilia vitunguu. Kuongeza kiwango cha majani ya mmea kunaweza kufanywa kwa kumwagilia kitunguu maji mengi kupitia mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone, pamoja na kuongeza mbolea kwenye maji ya umwagiliaji.
Baada ya kuweka bomba la kumwagilia, vitunguu hupandwa kwa safu mbili. Huku husaidia kwa sababu unaweza kutumia bomba moja la umwagiliaji kwa safu mbili za vitunguu.
Kulisha vitunguu
Jambo la pili muhimu katika kilimo cha vitunguu ni kulisha mmea. Vitunguu hupenda maji mengi na mbolea. Njia ya kwanza ya kulisha vitunguu ni kwa kuingiza mbolea kwenye mfumo wa umwagiliaji wa matone. Katika hatua za mwanzo, ingiza mbolea kwa viwango vya 20-20-20 kupitia njia ya matone.
Vitunguu vichanga huhitaji mbolea ya fosforasi na potasiamu ili kuhimiza ukuaji wa mizizi. Vinapokua vinahitaji tu nitrojeni.
Uwekaji mbolea
Vitunguu vinapokua, anza kutumia mbolea ambayo ni nitrojeni ya msingi kama vile nitrati ya chile. Unaweza pia kunyunyiza mbolea nitrati ya chile kando ya safu ya vitunguu.
Hatua ya kutoa vitunguu hudhihirishwa na pete nyingi zilizo kwenye kitunguu, na wakati huo maji mengi huhitajika ili kufanya kitunguu kiwe kikubwa.