Wakulima wote huzalisha nyanya katika wakati moja, na hivyo hupata hasara kutokana na bei ya chini wakikuta soko limejaa nyanya. Katika video hii, tunajifunza jinsi ya kupunguza hasara hizi kwa kuzalisha nyanya mwaka mzima.
Nyanya ni kiungo muhimu cha kupikia, na zinaweza kuliwa mbichi, kupikwa au kama nyanya nzito. Uzalishaji kwa wakati tofauti husaidia kupunguza hasara huu, na kuhakikisha uendeleaji wa kutoa nyanya za kutosha kila wakati. Unachohitaji ni utaalamu, aina sugu za mbegu zinazostahimili magonjwa na hali ya hewa, na upatikanaji wa maji ya umwagiliaji.
Uamuzi wa kikundi
Wakati kikundi cha wakulima wanapoamua kufanya upanzi wa wakati tofauti, wanakubaliana wakati muafaka ambapo kila mmoja wao anafaa kupanda. Baada ya hapo, wakulima hutumia ujuzi na maarifa yao kuzalisha nyanya. Wakati wa kufanya uzalishaji huo, umwagiliaji wa maji ni muhimu haswa katika wakati wa kutoa maua na matunda. Baada ya kuvuna, kikundi huamua kuhusu mkakati wa uuzaji. Ikiwa nyanya zitauzwa katika soko la mbali, huvunwa katika wakati hazijaiva vizuri. Zaidi ya hayo, kikundi pia kinajadili uzoefu wa kila mtu wakati wa uzalishaji. Ikiwa bei ni ndogo sana, wanaweza kuafikiana kuhifadhi nyanya.