Mbaazi ni zao kuu la chakula ambalo limekithiri protini na vitamini zinazotumika kama chakula cha mifugo, na kuongeza kipato na vile vile majani huliwa kama mboga.
Kupitia hatua sahihi za kilimo cha mbaazi, mavuno mengi hupatikana. Hata hivyo, ni muhimu kunyunyizia aina zinazoshambuliwa na vidukari kwa nyakati tofauti. Kwa mfano, nyunyizia dawa siku 14 hadi 21 baada ya kupanda. Baada ya mara ya kwanza ya kunyunyizia, nyunyizia tena baada ya siku 10. Kisha nyunyizia tena siku 10 baada ya kunyunyizia mara ya pili. Zaidi ya hayo, mbaazi hukua vizuri zaidi katika mvua iliyokati ya 500mm-1200mm. Aina zinazokomaa mapema hukua vyema katika mvua iliyochini ya 500mm kwa mwaka.
Hatua za kukuza mbaazi
Andaa ardhi kwa kufyeka, kuchoma takataka za shamba. Nyunyizia dawa za kuua magugu na kisha ulime na kulainisha udongo kwa ajili ya ukuaji sahihi wa mizizi, Panda mimea kwa muachano sahihi kulingana na aina ya mmea. Loweka mbegu kwenye maji usiku kucha ili kurahisisha kuota. Panda mbegu 2 – 3 kwa shimo na kwa kina cha sm 2- 5 ili kuziwezesha uotaji kwa urahisi. Punguza idadi ya miche hadi mimea 2 kwa kila shimo. Palilia mara mbili, yaani wiki 2 baada ya kupanda na wiki 4 – 5 baada ya kupanda ili kuhakikisha kwamba shamba halina magugu na hivyo kupunguza ushindani wa virutubisho.
Dhibiti wadudu na magonjwa kwa njia ya kibayolojia au kemikali kulingana na aina ya mbaazi ili kuongeza mavuno. Vuna wakati maganda ya mbegu yamekomaa na kukauka kulingana na aina ya mbaazi kwa vile aina tofuati za mbaazi hukomaa kwa nyakati tofauti. Hatimaye, pura maganda ya mbegu, na kuzisafisha. Tenganisha mbegu na makapi kwa njia ya kupepeta.