Wafugaji wengi wa kuku nchini Uganda hufuga kuku wa mayai, lakini kwa kiwango kidogo. Mbinu bora za usimamizi zinaweza kuongeza tija ya kuku wa mayai.
Kuku wa mayai wananweza kufugwa kwa mifumo mifumo miwili ili kuongeza uzalishaji wa mayai. Katika shamba, udhibiti na uzuizi wa uenezaji wa magonjwa ni muhimu sana.
Hatua za udhibiti na uzuizi wa uenezaji wa magonjwa
Ili kutekeleza jambo hilo shamba lako, unahitaji kuandaa sehemu ya kuulia viini kwenye mlango wa shamba ambapo mtu yoyote anayeingia lazima aoshe miguu yake. Pia, andaa sehemu ya kuchovya magurudumu ya gari kwenye dawa ya kuua viini.
Kwa ufanisi wa dawa, hakikisha kwamba michanganyiko ni sahihi na pia uzuie dawa isichafuke sana. Unaweza kufikia lengo hili kwa kuchovya miguu ya watu na magurudumu ya gari kwenye maji kabla ya kuchovya kwenye dawa.
Unaweza pia kusafisha mikono yako kwa kutumia dawa za kuua viini kabla ya kuingia kwenye banda la kuku, na pia kupunguza idadi ya wageni kwenye shamba kwa sababu hawa wanaweza kuwa chanzo cha maambukizi.
Hatua nyingine za usimamizi
Hakikisha msongamano sahihi wa kuku katika banda, mbao ni kati ya ndege 6 hadi 7 kwa kila mita mraba. Nafasi hii inajumuisha nafasi palipowekwa vihori.
Tolea kuku uwanja wa kutosha kufanyia mazoezi.
Uingizaji wa hewa unapaswa kuwa mzuri ili kuondoa hewa mbaya na kuingiza hewa safi.
Tolea ndege mwanga wa kutosha wa angalau masaa 16 kwa siku kwa sababu mwanga huchochea uzalishaji wa mayai.