Matunda ya maembe hukomaa kwa nyakati tofauti. kwa hivyo, kuvuna yote mara moja husababisha hasara. Uvunaji wa matunda yaliyokomaa pekee na utunzaji mzuri husababisha mavuno mengi pamoja na maembe bora.
Maembe hukomaa wakati tofauti kutegemea aina ya embe, hali ya rutuba ya udongo, na sababu zingine za kibinafsi. Matunda yaliyokomaa yana sifa na ishaara tofauti ambazo ni pamoja na; maua huanguka, sehemu ya juu huwa paana, eneo karibu na kijiti cha kujishukilia hubonyea ndani, ngozi ya matunda huwa na madoa, na kijiti cha kununginia nacho huanza kukauka. Lazima tuzingatie ishara hizi wakati wa kuvuna.
Bendera za rangi
Njia nyingine ya kutambua matunda yaliyokomaa ni kuweka bendera zenye rangi tofauti katika matawi yatakayotoa maua awali na mwisho. Tarehe ambayo kila kundi la maua lilianza kutolewa husajiliwa. Awali, vuna matunda kutoka kwa matawi yaliyotoa maua kwanza, na yale yaliyotoa maua baadaye huvunwa mwisho.
Hatua za uvunaji
Baada ya kukadiria ukomavu wa matunda kwa kutumia ujuzi wa nje, kata na kufungua sampuli za matunda ili kujua kiwango cha sukari kilicho katika tunda, pamoja na rangi ya tunda.
Tumia kifaa cha kupima kiwango cha sukari iliyo kwenye tunda. Hii hufanywa kwa kugawanya tunda katika sehemu 3 sawa. Kata sehemu ya kwanza hadi katika mbegu. Kisha likate kati ya mbegu na ngozi. Rekebisha kipimaji cha sukari na ukamue juisi ya tunda kwenye kipimaji. Elekeza kipimaji upande wa jua kisha usome kiwango cha sukari. Kipimo cha juu kinamaanisha sukari nyingi.
Vigezo vya ubora
Kiwango cha ukomavu wa kuvunia kinategemea aina ya embe na soko unalolenga. Masoko tofauti yanahitaji vigezo tofauti vya ubora wa embe.
Vuna maembe bila kuyaharibu. Hilo linawezekana kwa kutumia vifaa sahihi vya kuvuna kama nguzo za kuvunia. Hizi humuwezesha mvunaji kuchuma matunda kutoka kwenye miti na kuyaweka kwa upole kwenye kikapu. Hizi Pia huondoa vijiti vinavyo shikilia matunda ambavyo ni njia kuu ya kupitisha magonjwa, na pia hupunguza uwezo wa mti kutoa maua katika msimu ujao.
Pia kumbuka kila mara kuua viini kabla ya kutumia vifaa vya kuvuna ili kuzuia maambukizi ya magonjwa kutoka shamba kwenda lingine.
2 Responses
nahitaji kuwasilisha wazo langu katika kilimo cha matunda na nimawazo chanya yenye ubunifu wa hali ya juu
Tuna unyenyekevu kukusaidia katika eneo hili.