»Utunzaji mzuri wa nyanya«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/good-handling-tomatoes

Muda: 

00:06:30
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

Countrywise Communication

Baada ya kuvuna, ubora wa nyanya hupungua. Utunzaji mzuri wakati wa kuvuna na usafirishaji husababisha mapato bora.

Kupata nyanya bora huanza na jinsi kuvuna au kuchuma kunavyo fanyika. Chuma au vuna asubuhi wakati hali ya hewa ni baridi ili kuepuka kuharibika. Wakati wa kuvuna, chuma kwa uangalifu na uweke nyanya kwenye vikapu. Usitupe nyanya. Hifadhi nyanya kwenye kivuli baada ya kuchuma.

Kusafirisha nyanya

Afadhali tumia kreti za plastiki kwa usafirishaji wa nyanya. Zifunika ikiwa unatumia vikapu ili kuepuka uharibifu. Epuka kurunda nyanya ili kuokoa zile za chini kabisa. Hifadhi nyanya kwenye kivuli, na usivirushe vyombo vya kuhifadhi. Epuka kuweka nyanya moja kwa moja kwa udongo.

Tenganisha na kuchambua nyanya kabla ya kuzisafirisha ili kuondoa zilizoharibika na zilizopasuka. Kisha weka nyanya kwenye kreti au kikapu kwa uangalifu. Safirisha nyanya usiku au asubuhi mapema wakati joto liko chini.

Wakati wa kuvuna

Wakati wa kuvuna hutegemea kama nyanya ni za kuuza katika soko la karibu au la mbali. Kwa soko la karibu, vuna wakati nyanya ni nyekundu. Kwa soko la mbali, changanya nyekundu na zile zinazoanza kugeuka nyekundu.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:34Baada ya kuvuna, ubora wa nyanya hupungua.Hilo linaweza kutatuliwa kwa kutumia mbinu na hatua nzuri.
00:3501:29Kupata nyanya bora huanza na jinsi kuvuna kunavyo fanyika
01:3001:36Chuma au vuna asubuhi wakati hali ya hewa ni baridi.
01:3701:42Hifadhi nyanya kwenye kivuli baada ya kuchuma.
01:4302:21Hatua au wakati wa kuvuna hutegemea wakati wa kutumia.
02:2202:36Chuma nyanya kwa makiini na uziweke kwenye kreti.
02:3702:52Tumia kreti za plastiki kwa usafirishaji wa nyanya. Zifunika ikiwa unatumia vikapu.
02:5302:59Epuka kurunda nyanya.
03:0003:10Hifadhi nyanya kwenye kivuli, na usivirushe vyombo vya kuhifadhi. Epuka kuweka nyanya moja kwa moja kwa udongo.
03:1103:37Tenganisha na kuchambua nyanya kabla ya kuzisafirisha.
03:3803:57Vikapu husababisha uharibifu mkubwa.
03:5804:35Tumia trei za plastiki ili kupunguza uharibifu.
04:3604:49Weka nyanya kwenye kreti au kikapu kwa uangalifu. Baada ya kujazwa, weka vyombo katika mahali pakavu.
04:5005:39Kusafirisha nyanya kwenye trei za plastiki huleta fedha zaidi kuliko vikapu.
05:4006:30Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *