»Utumiaji wa mbolea ya majani«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=ZxxurjxzqTI&list=RDCMUC9U2fgUx3ybR8roC7RBR3YQ&index=6

Muda: 

00:08:42
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Mobile Tutor

Kwa kuwa ni moja wapo ya sekta kubwa duniani kote, kilimo kinaathiriwa zaidi na upungufu wa rutuba ya udongo, ambao husababisha uzalishaji duni.

Mbolea ya majani inahusisha uwekaji wa majani mabichi, vijiti vya miti, vichaka na mimea kwenye udongo. Hii ni teknolojia inayotumika kuboresha muundo wa udongo na rutuba yake.

Usindikaji wa mbolea

Katika teknolojia ya mbolea ya majani, majani na mimea ndio viambato vikuu vya kubadilisha muundo wa udongo na kuongeza mboji, nitrojeni na virutubisho vingine. Mchakato wa kutengeneza mbolea ya majani ni wa vitendo, endelevu na husaidia kiuchumi kwa kuongeza tija ya ardhi iliyotumika zaidi au isiyotumika.

Utekelezaji wa mbolea ya majani unategemea na hali ya hewa. Aina za mbolea ya majani pamoja na ile aina ambayo inahusisha na upandaji wa mazao kwenye kipande cha ardhi na kisha kuyakata yakifika hatua ya kuchanua maua. Mimea iliyokatwa huzikwa katika ardhi hiyo hiyo na baadaye huoza na kubadilia kuwa mboji. Katika aina ya pili, udongo huchanganywa na majani mabichi na matawi. Nyenzo huachwa nje kwa siku 2 na baadaye hukusanywa, hurundikwa na kufunikwa na majani ya migomba ili zioze. Nyenzo hizi huongezwa kwenye udongo na mchakato hurudiwa hadi udongo utakapofikia kiwango cha rutuba kinachohitajika.

Faida za mbolea ya majani

Green manuring improves on soil fertility, soil physical structure and addition of required nutrients which improve on soil aeration and its resistance to pests and diseases. Green manuring also controls weeds and stimulates microbial growth as well.

Changamoto za mbolea ya majani

Mbolea ya majani huboresha rutuba ya udongo, muundo wa udongo na kuongeza virutubisho vinavyohitajika. Kufanya huku huboresha uingizaji hewa wa udongo na uwezo wake wa kustahimili wadudu na magonjwa. Mbolea ya majani pia hudhibiti magugu na kuchochea ukuaji wa vijidudu muhimu.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0002:14Mbolea ya majani inahusisha uwekaji wa majani mabichi, vijiti vya miti, vichaka na mimea kwenye udongo.
02:1502:30Majani na mimea ndio viambato vikuu vya kubadilisha muundo wa udongo.
02:3102:44Mbolea ya majani huongeza nitrojeni na virutubisho vingine kwenye udongo
02:4503:54Mchakato wa kutengeneza mbolea ya majani ni wa vitendo, endelevu na husaidia kiuchumi.
03:5504:00Utekelezaji wa mbolea ya majani unategemea na hali ya hewa
04:0104:10Aina za mbolea ya majani
04:1105:43Kuna aina ambayo inahusisha na upandaji wa mazao kwenye kipande cha ardhi na kisha kuyakata yakifika hatua ya kuchanua maua, na kuyazika katika ardhi hiyo hiyo.
05:4406:55Katika aina ya pili, udongo huchanganywa na majani mabichi na matawi
06:5607:10Mbolea ya majani huboresha rutuba na muundo wa udongo
07:1107:28Huboresha uingizaji hewa wa udongo na uwezo wake wa kustahimili wadudu na magonjwa.
07:2907:38Hudhibiti magugu na kuchochea ukuaji wa vijidudu muhimu.
07:3907:56Changamoto: mbolea ya majani huchukua muda mrefu, na haifai kwa mazao yanayotegemea mvua.
07:5708:03Gharama ya utekelezaji ni kubwa
08:0408:42Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *