Usindikaji wa mvinyo
Kwanza, osha vifuniko ili kuondoa vumbi kabla ya kuvitumia. Usiloweke ndani ya maji kifuniko kinachotumika kufunika chupa ya mvinyo. Kuna aina mbalimbali za vifuniko ambazo ni pamoja na knock on corker, corker 2 handler corker n.k.
Vile vile, weka lebo kwenye chupa, na kila mara hafadhi chupa zikisimama wima baada ya kuwekea kifukino kwa siku 3 za kwanza . Baada ya siku 3, hifadhi chupa zilizo na mvinyo kwa upande mmoja ili kifuniko kiwe na unyevu. Weka kifuniko kingine juu ya kizibo ili kuzuia uvujaji. Hatimaye, weka mvinyo kwenye demijohns ili uweze kukomaa.