Mitende hushambuliwa sana na wadudu na magonjwa kadhaa. Waakini kupogoa, kupanda mseto na kupalilia kunaweza kusaidia kuzuia magonjwa haya na wadudu.
Kupogoa ni moja wapo ya shughuli za kimsingi, ambazo huzuia wadudu kutaga mayai kwa matawi ya mitende. Kupogoa pia hurahisisha mchakato wa kupanda mitende. Kupogoa hufanywa kwa kutumia kisu maalum wakati wa masika, ambapo mimea ina unyevu wa kutosha. Hii hurahisisha mchakato wa kupogoa.
Kupanda mseto
Kupanda mseto wa mitende na mboga maalum husaidia kuvutia maadui wa asili (wadudu) ambao hula wadudu wa mitende na mayai yao. Mabaki na takataka ya mboga inaweza kuchanganywa na udongo ili kuongeza rutuba ya udongo.
Palilia chini na karibu ya mitende ili kuondoa magugu. Magugu husababisha athari kubwa katika uzalishaji kwa kuhifadhi wadudu na magonjwa. Magugu pia kushindana na mimea kwa maji na virutubisho, na pia huongeza unyevu unaosababisha kuvu.
Kufanya hatua hizi kunaweza kuongeza uzalishaji wa mitende, ubora, ukubwa wa matunda , na kuharakisha ukomavu wa mmea. Kwa hivyo, huongeza mapato ya kiuchumi. Hatua hizi pia hupunguza matumizi ya kemikali kudhibiti wadudu.