»Usimamizi wa kulisha ndama«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=qWpd6s-D3hY

Muda: 

00:08:13
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Digital Agriculture

Ndama huhitaji usimamizi mzuri ili kukua vyema, kwa hivyo wafugaji wanapaswa kuzingatia kanuni za kimsingi za usimamizi ili kuongeza uzalishaji.

Ulishaji sahihi wa ndama huwasaidia kukua wakiwa na afya njema, pamoja na kufikia ukomavu wa mapema wa kijinsia. Hii huongeza kipato endelevu na bidhaa bora za mifugo. Kwa hiyo, inapendekezwa kila mara kwa wakulima kufuata taratibu hizi za usimamizi.

Mbinu za usimamizi

Daima walishe ndama maziwa ya kwanza (kolostramu) katika siku za kwanza ili kuongeza kinga ya ndama dhidi ya magonjwa, kisha walishe ndama ukitumia chupa.

Pili, mfunze ndama kulishia kwenye ndoo ili aweze kunywa maziwa mazuri kwa kiwango cha moja ya kumi ya uzito wa mwili wake.

Wape ndama chakula cha kuanzia wakiwa na umri wa siku 15 hadi miezi 3 ili kuongeza kiwango cha nishati na pia kuboresha ukuaji wa tumbo.

Baada ya miezi 3 wape ndama chakula cha mkusanyiko cha kutosha ili kuongeza viwango vya nishati.

Mwisho, wape ndama mchanganyiko wa madini na virutubisho vya vitamini kwukuaji wa jumla na pia wape maji safi ya kunywa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:06Ulishaji sahihi wa ndama huwasaidia kukua wakiwa na afya njema, pamoja na kufikia ukomavu wa mapema wa kijinsia.
01:0702:39Daima walishe ndama maziwa ya kwanza (kolostramu) katika siku za kwanza, kisha walishe ndama ukitumia chupa.
02:4003:36Mfunze ndama kulishia kwenye ndoo.
03:3704:16Wape ndama chakula cha kuanzia wakiwa na umri wa siku 15 hadi miezi 3
04:1705:30Baada ya miezi 3 wape ndama chakula cha mkusanyiko cha kutosha
05:3107:12Wape ndama mchanganyiko wa madini na virutubisho
07:1308:13Pia wape maji safi ya kunywa.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *