Samaki ni muhimu kwa wafugaji wengi kwani hutoa chakula, mapato na ni chanzo cha protini kwa walaji. Hata hivyo ukuaji wake huathiriwa na wawindaji, na hivyo huhitaji mbinu sahihi za usimamizi wa mabwawa.
Wakati wa kulisha samaki, epuka kuwalisha wakati wa mvua, asubuhi sana, wakati wa baridi na wakati wa giza. Epuka kuweka madini mengi sana katika bwawa, kwani haya huzuia upenyaji wa mwanga, jambo ambalo linaweza kuzuia ukuaji wa malisho asili ya samaki.
Hatua za a usimamizi
Fyeka nyasi iliyo karibu na bwawa mara kwa mara, pia dumisha ulinzi wa bwawa kwa kuweka nyavu, uzio, na kufuga mbwa ili kuzuia wavamizi. Linda samaki dhidi ya chura, nyoka, mijusi, kobe, na ruba kwani wanaweza kuvamia na kula samaki, na hivyo kupunguza idadi ya samaki.
Fyeka nyasi kwenye njia ya kuingilia na kutoa maji kwenye bwawa, ili kudhibiti wawindaji, na kuongeza mtiririko kasi wa maji ili kuzuia uingiaji wa ruba kwenye bwawa. Vile vile, ondoa nyasi zinazochipuka ili kuzuia mayai ya chura na chura wachanga kupata mahali pa kujishikanisha. Kisha safisha mifereji ya maji ili maji yaweze kupata hewa, na hivyo kuongeza kiasi cha oksijeni katika maji.
Kushughulikia upepo
Lisha samaki vizuri kwa kutumia pellets au vyakula vya unga. Hata hivyo, vyakula vya unga hupeperushwa kwa urahisi na upepo yaani uangalifu unapaswa kuzingatiwa wakati wa kulisha samaki. Weka madini au virutubisho kwenye bwawa mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa maji yanakuwa na rangi ya kijani kibichi ambayo hutoa chakula cha asili kwa samaki, pamoja na kuzuia samaki wasionekane na wawindaji.