Bakajani ( bacterial leaf blight) inaweza kuharibu hadi nusu ya mavuno yako. Kwa hivyo ni muhimu kujua jinsi ya kuzuia ugonjwa huo.
Bakajani huonekana sana katika mwanzo wa msimu, na husambaa hasa kupitia kwenye mbegu, vidonda, maji ya mvua na maji ya umwagiliaji. Unapopanda aina majo kila mwaka, ugonjwa huo unaweza kuwa na mlipuko mkubwa. Bakajani hupatikana pia kwenye magugu, na mapaki ya mazao na inaweza kushambulia mavuno yako kuto kwenye hayo.
Bakajani ya bakteria
Ugonjwa huu huathiri mimea ya mpunga katika kitalu na zao kuu la shamba. Unaweza kuitambua, kwa sababu ncha ya majani ya mpunga hukauka. Kisha bakajani huenea chini ya upindo wa majani. Bakajani huonekana kama hali ya muundo wa wimbi. Mwishowe hukausha mmea wako.
Unapotaka kuangalia ikiwa mimea yako ina ugonjwa, unaweza kukata majani yalio na ugonjwa na kuiweka kwenye kikombe kilichojazwa na maji. Ikiwa majani hutoa majimaji ya hudhurungi ambayo hutokana na bakteria, unajua kuwa mimea yako imeathiriwa. Hii haimaanishi kwamba mimea yako yote itaugua, bali ugonjwa unaweza kuharibu karibu nusu ya shamba. Kutoka umbali kadha, unaweza kuona vizuri ni mimea mingapi imeathiriwa.
Usimamizi wa ugonjwa
Ili kudhibiti ugonjwa, panda mbegu zilizo na afya, na sugu dhidi ya ugonjwa wa bakajani. Unafaa daima kuondoa magugu na mabaki ya mazao shambani lako na uyaoze.
Baadaye katika msimu,usikate majani yaliyoathiriwa, kwa sababu hapo ugonjwa unaweza kuenea kwa urahisi. Virutubisho kama zinc na copper husaidia kujenga mmea na kuufanya uwe sugu zaidi.
Mara tu unapogundua majani makavu, unafaa kuchanganya kilo 40 za samadi mbici ya ng‘ombe na lita 100 za maji kwa nusu hekta. Acha ikae kwa masaa 24. Kisha koroga samadi na uchuje kwa mfuku. Baadaye unaweza kuongeza lita 100 za maji. Nyunyizia mchanganyiko huo kwa siku 15, kila siku mara tatu.
Unaweza pia kutumia kilo 1 ya Pesudomonas-talc kutoka dukani, na lita 200 za maji kwa nusu hekta. Tumia mchanganyiko huu siku 15 baada ya kupandikiza. Siku 10 baadaye, nyunyiza tena, na kisha baada ya siku 10 nyingine ongeza kunyunyiza mchanganyiko huo.