Ugonjwa wa uozo (kuoza mizizi) na ukungu mweupe (kuoza mashina) huathiri sana njugu, na kupunguza mavuno. Ukungu mweupe huenezwa kupitia hewa, na maji ya umwagiliaji. Lakini maji yaliyotuama hueneza magonjwa yote mawili.
Utambuzi wa mapema, udhibiti sahihi na hatua sahihi za uzuiaji husababisha mavuno mazuri. Njugu hupandwa sana, na hutumiwa kutengeneza mafuta ya kupikia, ni chanzo cha lishe la ng‘ombe na kuku, mbolea za kikaboni, na kuongeza rutuba ya udongo kwa kuongeza nitrojeni.
Ishara na dalili za ukungu mweupe ni: Mimea hukauka na kunyauka, na mizizi ina harufu mbaya. Ukungu mweupe hutokea siku 30 baada ya kupanda. Ugonjwa huo husababishwa na kuvu inayoishi katika udongo.
Udhibiti na uzuiaji
Kwanza, Lima udongo kwa kina ili kuleta mchanga juu ambapo jua linaweza kuua kuvu. Panda kwenye vitalu vilivyoinuliwa (15 cm juu) ili kuondoa maji ya ziada. Pili, tumia kuvu yenye faida kwa ufyonzaji wa virutubisho zaidi. Palilia mimea ili iweze kunasa jua na hewa zaidi.
Kwa kuongeza ng‘oa na kuchoma mimea iliyoathiriwa ili kuzuia kuenea kwa magonjwa. Nyunyiza dondoo au mchanganyiko wa mbangimwitu ili kuthibiti mimea dhidi ya ugonjwa. Tumia jasi la unga kudhibiti uozo. Baada ya kuvuna panda mimea tofauti ili kuzuia kuongezeka kwa kuvu kwenye udongo.