Kwa kuwa ni jambo muhimu la ukuaji wa mazao, kiwango cha umwagiliaji kinaamuliwa na aina ya mazao, msimu na uwezo wa mkulima kununua vifaa.
Katika umwagiliaji kwa njia ya mtaro, mabomba husukuma maji kwenye mitaro, na mabomba ya kipenyo cha inchi 6 na urefu wa futi 20-30 hutumiwa. Tundu huwekwa kila baada ya inchi 30 kwenye bomba la umwagiliaji, matundu haya huwezesha maji kutiririka ndani ya mtaro.
Uanzishaji wa mfumo
Umwagiliaji kwa njia ya mtaro huruhusu mtiririko wa maji katika mwelekeo mmoja, mfumo pia huruhusu utumiaji wa trekta kudhibiti magugu. Tumia mazao ambayo yana mizizi ya kina kirefu kwa ufyonzaji mzuri wa maji. Hatimaye, mwagilia kwa kutumia mfumo wa mitaro baada ya kila siku 10 au wiki 2 kulingana na aina ya udongo.