Uzalishaji wa muhogo huathiriwa zaidi na magonjwa mawili; ugonjwa wa batobato(CMD), na matekenya (CBSD). Matekenya huathiri mmea mzima na naweza kusababisha hasara kubwa sana.
Ugonjwa matekenya huenezwa na wadudu kwa mfano nzi weupe. Visu vinavyotumika kukata mashina ya muhogo ulioathirika pia hueneza ugonjwa huo vikitumika kukata shina la muhogo wenye afya, na wakati shina la mmea ulioathirika linapogusana na shina la mmea wenye afya hasa wakati wa upepo.
Dalili za ugonjwa wa matekenya
Dalili za ugonjwa wa matekenya huonekana kwenye majani, mashina na mizizi.
Majani hugeuka manjano, michirizi ya kahawia/michibuko kwenye shina, na katika hali mbaya mmea hukauka kutoka kwenye ncha kwenda chini. Dalili muhimu zaidi ni zile zinazoonekana kwenye mizizi. Umbo la mzizi hupinda na sehemu ya ndani ya mzizi inayoweza kuliwa huonekana kahawia, huoza na huwa ngumu.
Ugonjwa huo huenezwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa na kupitia eneo la kuzidishia mbegu, iwapo chanzo asili kiliambukizwa.
Udhibiti wa matekenya
Kwa kuanzia, usimamizi ni kuhakikisha unapanda vipandikizi vya mihogo isiyo na magonjwa. Epuka kugawana vifaa vya shambani kwani haku kunaweza kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo kutoka shamba moja hadi jingine. Panda aina za mihogo inayostahimili magonjwa. Mimea iliyoambukizwa inapaswa kung‘olewa na kuharibiwa kwa kuwa ni chanzo cha viini vinavyosababisha ugonjwa huo.
Wakati wa kuzidisha vipandikizi vya muhogo, ukaguzi wa shamba kwa ugonjwa wa matekenya ufanyike na wafanyakazi wenye ujuzi.