Kwa kuwa ni biashara nzuri, ubora wa wingi wa bidhaa za ng‘ombe hutegemea mbinu za usimamizi zinazotumika.
Ufugaji wa ng’ombe ni biashara yenye faida kubwa. Ili kuanzisha ufugaji wa ng’ombe, unahitaji kuandaa mpango wa biashara, kuamua juu ya ukubwa wa mradi na muda, pamoja na idadi ya ng’ombe, eneo na lengo la soko.
Usimamizi wa ng‘ombe
Anzisha biashara kwa kiwango kidogo, na endelea kuipanua kwa muda. Kisha zingatia bei ya ngombe sokoni, aina ya ng‘ombe na umri. Hakikisha kwamba kuna pesa za kununua ng‘ombe kila wakati.
Vile vile jenga banda lililo na paa la mabati, sakafu ya saruji na vihori vya chakula. Banda linapaswa kuwa wazi upande mmoja, na liwe karibu na nyumba ya mkulima. Tolea mnyama nafasi ya kutosha, na endelea kumpa malisho bora kwa unenepeshaji wa ng‘ombe.
Kiasi cha chakula kinachotolewa hutegemea uzito na umri wa ng‘ombe na kwa hili, toa wastani wa kilo 8–15 za malisho kwa kila mnyama kwa siku. Idadi ya wafanyakazi hutegemea ukubwa wa mradi wa ufugaji wa ng‘ombe.
Hatimaye, kuna haja ya kuwa na ujuzi wa kitaalam wa ufugaji wa ngombe ili kufanikiwa na biashara. Uza nyama ya ng’ombe nyumbani, bucha, shuleni, mikahawani, na madukani makubwa.