»Ufugaji wa kuku wenye faida«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=DqjPKaYJSEI

Muda: 

00:10:22
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

AIM Agriculture

Kibiashara, wafugaji wengi wa kuku hufuga kuku wa mayai au kuku wa nyama, lakini wengi wanashangaa ni biashara gani kati ya hizo mbili ina faida zaidi ikilinganishwa na nyingine.

Kuanzisha na kusimamia ufugaji wa kuku wa mayai huonekana kuwa rahisi, lakini ufugaji wa kuku wa nyama ni rahisi ikilinganishwa na wa kuku wa mayai. Ili kuanzisha ufugaji wa kuku wa nyama, unahitaji gharama ndogo tu ya uwekezaji yaani unahitaji chakula tu kuanzia siku ya 1 hadi wiki ya 6, chanjo chache, na shughuli chache za usimamizi ikilinganishwa na kuku wa mayai ambao huhitaji gharama kubwa ya uwekezaji, hulishwa kwa miezi 4 kabla ya kutaga mayai, huhitaji chanjo nyingi na kadhalika.

Kuku wa nyaka wakilinganishwa na kuku wa mayai

Katika mtazamo wa kibiashara, ufugaji wa kuku wa nyama hutoa mapato mapema ikilinganishwa na kuku wa mayai. Walakini, kuku wa mayai huto mapato mengi kwa ujumla ikilinganishwa na kuku wa nyama.

Ufugaji wa kuku wa nyama una hatari ndogo ikilinganishwa na kuku wa mayai.

Kuna faida kidogo kwa kila ndege katika kuku wa nyama, lakini hizi zinaweza kuongezwa kwa kutotolesha vifaranga wako mwenyewe na kutengeneza malisho yako badala ya kutegemea tu chakula kilichonunuliwa kutoka kwenye maduka ya malisho.

Mkakati wa uuzaji unaweza kuongeza mapato kutoka kwa kuku wa mayai na kuku wa nyama. Mfugaji wa kuku ambaye huongeza thamani ya kuku wake kama vile kuwachinja na kuuza katika soko bora hupata faida zaidi kuliko yule anayeuza kwenye soko la kawaida. Ili kupata kipato zaidi, fanya uchunguzi wa soko, zingatia gharama ya uzalishaji na tengeneza malisho ya kuku wako mwenyewe.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:28Ufugaji wa kuku wa nyama ni rahisi ikilinganishwa na wa kuku wa mayai.
00:2900:48Ili kuanzisha ufugaji wa kuku wa nyama, unahitaji gharama ndogo tu ya uwekezaji.
00:4901:25Kuku wa mayai huhitaji gharama kubwa za uwekezaji
01:2603:10Ufugaji wa kuku wa nyama hutoa mapato mapema ikilinganishwa na kuku wa mayai.
03:1104:53Ufugaji wa kuku wa nyama una hatari ndogo ikilinganishwa na kuku wa mayai.
04:5406:30Kuna faida kidogo kwa kila ndege katika kuku wa nyama
06:3106:44Totolesha vifaranga wako mwenyewe na kutengeneza malisho yako ili kuongeza mapato.
06:4509:30Mkakati wa uuzaji unaweza kuongeza mapato kutoka kwa kuku wa mayai na kuku wa nyama.
09:3110:22Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *