Kwa kuwa ni biashara nzuri, ubora wa wingi wa bidhaa za kuku hutegemea mbinu za usimamizi zinazotumika.
Ufugaji wa kuku wa nyama ni biashara yenye faida inayofanywa hasa kuzalisha nyama na katika hili, mahitaji ya wafanyakazi ni kidogo ikilinganishwa na biashara nyingine za mifugo kama vile ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na ng‘ombe wa nyama.
Usimamizi wa kuku
Ili kujenga banda la kuku wa nyama, kuna haja ya kuchagua mahali pasipotwamisha maji, penye hewa ya asili ambayo husawazisha halijoto ya ndege. Endelea kupunguza halijoto kwa kujenga nyumba katika uelekeo wa mashariki-magharibi ili kupunguza upenyaji wa jua moja kwa moja ndani ya nyumba.
Vile vile, toa nafasi ya kutosha, yaani mita ya mraba 1 kwa kuku 10. Nunua vifaranga wa siku moja kutoka kwa wauzaji wanaoaminika kwani mafanikio ya mradi wa kuku hutegemea aina ya vifaranga wa siku moja wanaoletwa. Kagua ubora wa vifaranga kwa kuangalia kama ni wasafi, wakavu, wana macho angavu na hawana ulemavu.
Kuku wa nyama huuzwa wakiwa na umri wa wiki 6 na katika hili, kila ndege hutumia kilo 4 za chakula kutoka wiki 0–6, na kwa wakati huu watakuwa na kati ya kilo 2.2 hadi 2.5. Kuku hulishwa kulingana na hatua ya uzalishaji. Malisho ya kuku hujumuisha chakula cha kuanzia, chakula cha kuku wanaokua na chakula cha kumalizia. Kuku huhitaji maji ya kutosha kwa ukuaji mzuri.
Endelea kuwatolea chakula cha nyongeza juu ya malisho ili kudhibiti mafadhaiko. Hatimaye, uza kuku kwenye masoko yanayopatikana.