»Udhibiti wa vichaka nchini Namibia. Kugeuza kichaka kuwa malisho«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=wfCaatiMDV0

Muda: 

00:07:40
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

De-bushing Advisory Service Namibia

Wakati wa ukame, malisho huwa ni changamoto kubwa linalowakabili wafugaji katika ufugaji wa wa mifugo yao. Hii hupunguza ubora wa bidhaa za mifugo na vile vile huathiri uzalishaji.

Chakula cha ya mifugo kutoka kwenye vichaka asili ni fursa kubwa kwa wakulima wanapopata malisho kutoka vichakani huku wakidhibiti ukuaji wa vichaka shambani mwao. Chakula cha mifugo kutoka vichakani hutumika sana hasa katika wakati wa ukame kama chakula cha dharura na kama chakula cha ziada.

Uzalishaji wa malisho

Kwanza, kichaka huvunwa kikiwa kibichi, na huvunwa pamoja na maua, majani na mbegu zake kwa kutumia panga. Matawi membamba hutumika kutengeneza malisho bora. Baada ya kuvuna, matawi na machipukizi husagwa kuwa nyuzinyuzi ambazo huchanganywa na virutubisho na kisha kulishwa kwa mifugo papo hapo.

Vile vile, katika uhifadhi, nyuzinyuzi hukaushwa kabla ya kuchanganya na madini. Malisho ya vichakani ni suluhuhisho katika kipindi cha kiangazi au ukame, na pia ni biashara nzuri.

Uzalishaji wa malisho ya vichakani hupunguza utegemezi wa malisho kutoka nje na kwa muda mrefu, huchangia katika urejeshaji wa nyanda za malisho.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:01Chakula cha ya mifugo kutoka kwenye vichaka asili ni fursa kubwa kwa wakulima kulisha mifugo yao.
01:0202:05Wafugaji hupata malisho kutoka vichakani huku wakidhibiti ukuaji wa vichaka shambani mwao.
02:0602:22Chakula cha mifugo kutoka vichakani hutumika sana hasa katika wakati wa ukame kama chakula cha dharura na kama chakula cha ziada.
02:2303:30Kichaka huvunwa kikiwa kibichi kwa kutumia panga
03:3104:01Matawi membamba hutumika kutengeneza malisho bora.
04:0204:09Baada ya kuvuna, matawi na machipukizi husagwa kuwa nyuzinyuzi.
04:1004:15Nyuzinyuzi huchanganywa na virutubisho na kisha kulishwa kwa mifugo papo hapo.
04:1604:22Vile vile, katika uhifadhi, nyuzinyuzi hukaushwa kabla ya kuchanganya na madini.
04:2305:26Malisho ya vichakani ni suluhuhisho katika kipindi cha kiangazi au ukame, na pia ni biashara nzuri.
05:2705:41Uzalishaji wa malisho ya vichakani hupunguza utegemezi wa malisho kutoka nje.
05:4207:30Kwa muda mrefu, huchangia katika urejeshaji wa nyanda za malisho.
07:3107:40Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *