Ugonjwa wa kiwele ni vimbe wa kiwele cha mnyama unaodhihirishwa na mabadiliko ya kiwele na maziwa kimwili, kikemikali na kibaolojia.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria kupitia mazingira ya ukamuaji yasio safi. Hata hivyo, unaweza kudhibitiwa kwa kufuata kanuni za usafi za ukamuaji. Kwa hivyo ni muhimu kutambua na kudhibiti ugonjwa huo ili kupunguza hasara ya kiuchumi. Ni muhimu kusafisha kiwele kilichoathiriwa kabla ya uchunguzi. Tumia kikombe cha kupima ugonjwa.
Dalili
Kuna dalili nyingi za ugonjwa wa kiweleambazo ni pamoja na, uvimbe wa kiwele, mabadiliko ya rangi ya maziwa, maziwa huganda, uwepo wa damu kwenye maziwa, uwepo wa usaha, ugumu wa kiwele, kupunguka kwa kiwango cha maziwa, homa, na ulaji mdogo wa chakula.
Matibabu
Kamua maziwa yote kutoka kwa kiwele kilichoathiriwa baada ya uthibitisho wa kuwepo kwa ugonjwa ili kuimarisha matibabu zaidi.
Weka viuavijasumu ndani ya matiti yaliyoathiriwa kwa matibabu bora.
Hatua za udhibiti
Kamua wanyama walioambukizwa mwisho ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa kwa wanyama ambao hawajaambukizwa.
Vile vile osha mikono vizuri kabla na baada ya kukamua. Usiruhusu mnyama kulala chini baada ya kukamua ili kuepuka maambukizi kwa matiti.
Hatimaye kusanya maziwa ya kwanza ya kila titi kivyake ili kuwezesha upimaji sahihi wa ugonjwa.